ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 14, 2013

Naibu Waziri wa Fedha afungua mkutano wa kikao kazi, Bagamoyo

Naibu Waziri wa Fedha ,Mhe. Saada Salum Mkuya akifungua mkutano wa kikao kazi unaofanyika hapa mjini Bagamoyo kwa muda wa siku mbili. Kikao kazi hicho kitakuwa na jukumu kubwa la kujadili ripoti ya kutathmini utendaji kazi wa mfumo wa usimamizi wa fedha za umma ambayo imeshakamilika( PEFA Report). Lengo kubwa la kikao hicho ni kutafuta ufumbuzi wa matatizo ambayo yamebainishwa katika ripoti hiyo. Kikao hicho kitawashirikisha washirika wa maendeleo pamoja Wizara ya fedha yenyewe.
Wa kwanza kushoto ni Bw. Gauthier Dewoelizent – BTC, wa katikati ni Bw. Layson N. Mwanjisi ambaye ni Mhasibu Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Ndugu Stanley Haule ambaye ni mkurugenzi msaidizi kutoka idara ya mifumo ya kompyuta Wizara ya fedha wakisikiliza kwa makini mada na maoni yaliyokuwa yakitolewa katika kikao hicho. Picha na kitengo cha Mawasiliano - Hazina
Janne Rajpar mwenyekiti mwenza kwa upande wa wahisani katika kusimamia matumizi ya fedha za umma kutoka ujerumani.
Kutoka kushoto ni Bi Ingiahedi Mduma ,ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano serikalini, wakatikati ni Bi. Hannah Mwakalinga kutoka PPRA ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za kiushirikiano na wakushoto kwake ni Bw. Malima Nkilijiwando ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Mipango kutoka Kwa Mkaguzi mkuu wa Mahesabu, wakisikiliza kwa makini mada na maoni yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo
Wa kwanza kushoto ni Bw. Sebastian Ndandala ambaye ni Kaimu msimamizi wa mradi wa maboresho ya fedha za umma( PFMRP) kwa upande wa serikali na anayefuata ni Bi. Paddy Siyanga Knudsen ambaye ni msimamizi kwa upande wa Washirika wa maendeleo,wakisikiliza kwa makini mada na maoni yaliyokuwa yakitolewa katika kikao hicho
Juma Salumu Maguru Mkurugenzi Msadizi idara ya Mipango Wizara ya fedha akitoa utangulizi kwa washiriki wa kikao hicho, hawapo kwenye picha.
Prof.Adolf F Mkenda Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha akitoa mada kwa washiriki wa mkutano huo, hawapo kwenye pcha.
Naibu Waziri wa Fedha ,Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Serikali ya Tanzania pamoja na Washirika wa maendeleo kutoka nchi Wahisani.

No comments: