ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 15, 2013

PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR,AAMUA KUSEMA UKWELI NAMNA ALIVYOISHI KWENYE MAJARIBU KABLA YA TUKIO

Siku moja baada ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang’amba kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana, imebainika kuwa alitishiwa kuuawa miezi mitatu kabla ya kukutwa na tukio hilo. 
Wakati Padri huyo akieleza hayo, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ameijia juu polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini na serikali visiwani humo, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku akilitaka kuwakamata waliohusika na tukio hilo.
Kiongozi huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali hiyo alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la Coastal kutoka visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Dk Shein alisema Polisi inatakiwa kuongeza nguvu za uchunguzi ili kukabiliana na matukio ya kikatili ya umwagaji wa tindikali, yanayoshamili visiwani humo hivi sasa.
“Hatuwezi kuviacha vitendo hivi viendelee … ni lazima Jeshi la Polisi lijitahidi kuwatafuta wahusika ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Dk Shein.
Dk Sheni alisema, kitendo hicho ni cha kikatili na kisichovumilika na kuongeza kuwa wahusika lazima wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake, Padri wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Zanzibar, Thomas Assenga aliyefuatana na kiongozi huyo mpaka MNH, alisema siku za nyuma Padri Mwang’amba alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati akienda kutoa huduma katika kituo cha wazee cha Welezo.
Alisema kabla ya kufika kituoni hapo, kuna eneo ambalo nyakati za asubuhi watu hufanya mazoezi barabarani ambapo kuna mtu mmoja alimtolea maneno ya vitisho.
“Unajua kawaida ya watu wa Zanzibar hufanya mazoezi barabarani, sasa kipindi anapita eneo hilo katika kilima, kuna mtu alimwambia atamfanyia kitu kibaya ambacho hatujui ndiyo hiki au la,” alisema Padri Assenga na kuongeza:
Alisema Juni mwaka huu mara baada ya kupewa vitisho hivyo alikwenda kutoa taarifa kwa Sheha wa eneo hilo na kituo cha polisi.
“Mara baada ya kutolewa vitisho hivyo Juni mwaka huu, alichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mkuu wa eneo hilo (Sheha) na kituo cha polisi.”
Akielezea tukio la kumwagiwa tindikali Padri Mwang’amba, alisema alimwagiwa saa 9:45 alasiri juzi wakati akizungumza na simu nje ya internet café iliyopo eneo la Mlandege.

4 comments:

Anonymous said...

wenye akili wajiulize mbona toka zamani vituko kama hivi na matukio kama haya yalikuwa hayapo kwa nini ya wepo hivi sasa nini kinachopikwa katika chungu au kwa vili wazanzibari hawautaki muungano ndo maana kila baya wanazuliwa hivi sasa mungu ndo ajuaye na ndo atakaye walipia wanoa taka kuyazamisha mamlaka kamili ya zanzibar na mungu pia atawalipia walio mfanyia unyama huu padri vimbo ya mungu kali jamani iuogopeni msiwe mnazuoa migogoro na matukio kila leo na kuchafua hali ya hewa ya amani ya visiwa vya karafuu zanzibar

wazanzibari hawana hulka hizi jamani muogopeni mungu jamani

NEW ORLANDO

Anonymous said...

mamlaka kamil ya watu wa zanzibar yatakuja tu mungu akipenda bila hiyana wala ufisadi wenu wa kupakazia maovu ambayo wazanzibari hawana hulka na desturi nayo amin, mungu tusaidiye tupate nchi yetu amin

Anonymous said...

Acheni kujisafisha nyie waznz sasa mnataka kuniambia kuwa ni wabara hao? Don't u dare lying.....!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Na kiukweli mnajua kabisa bila TZ bara nyinyi ni nothing, hamuwezi bila muungano mnapoteza Muda bureeee.

Anonymous said...

Tatizo kubwa la zanzibar ni kuwa na per capita illiteracy rate kubwa sana barani Afrika. Serikali inabidi kujenga shule za kutosha ili kuwasomesha vijana,if possible wapate free education kama ilivyokuwa bara in the 1970s-80s. Kuwafundisha watoto katika shule za madrasa/Quran is not good enough. Kama tutawaelimisha young zanzibaris, nina imani tutapunguza vitendo vya ukatili, upumbafu, na na vurugu in the near future. Unfortunately, ndugu zetu wa Zanzibari are very slow in catching up with globalisation, wanahitaji ELIMU ili kujikwamua, otherwise kitakuwa ni kisiwa chenye raia wengi wapumbafu hata kama watatoka kwenye serikali ya Muungano. I am sure sisi wa bara tunaweza kuliokoa jahazi kwa kuwasaidia hawa wenzetu, maana tunao wasomi wengi zaidi!Binafsi, nipo tayari kutoa mchango hivyo, nawaomba wadau wasomi wenzangu wengine mliopo ughaibuni mjiunge .