Kwa wasomaji wa blog / tovuti hii
SALAAM
Nimeamshwa na taarifa juu ya malalamiko ya MMK MEDIA kwenye vyombo vya habari kuhusu ubalozi na / ama afisa balozi wake
Binafsi napenda kugusia mambo mawili kuhusiana na lalamiko lao KWA NAMNA AMBAVYO NIMEHUSISHWA / TUMEHUSISHWA (kama Jamii Production)
Katika malalamiko hayo, MMK MEDIA imeambatanisha BARUA YANGU ambayo ilikuwa ni BARUA BINAFSI KWA KAIMU BALOZI (kwa wakati huo) Mama Lilly Munanka.
Barua hiyo (kama nilivyosema hapo awali) ilikuwa ni BARUA BINAFSI na haikupaswa kuchapishwa kwenye blogu kama ilivyotokea. Niliiandika kwa Mama Munanka kama barua ya awali ya malalamiko kwake na haikuwa barua ya kuchapisha kwenye blogu kama ilivyotokea (kwa bahati mbaya) kwa wale niliowaambatanisha.
KAMA INGEKUWA NI YA KUCHAPISHWA KWENYE BLOGU, BASI INGEKUWA KWENYE BLOGU YANGU KABLA YA KWINGINE KOKOTE
Hata hivyo, punde baada ya kuchapishwa niliwasiliana na wanahabari wenzangu (ambao niliwaambatanisha katika barua hiyo) na kuwaeleza kuwa ile ilikuwa NAKALA KWAO NA SIO CHAPISHO LA BLOG.
Nilifanya hivyo kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuwasiliana na Mama Munanka na hivyo halikuwa jambo sahihi kuchapisha barua hiyo bloguni.
Lakini pia, katika lalamiko la sasa, MMK MEDIA wameandika kuwa "Baada ya tukio hafla hiyo kubwa kupita bila kusita niliandika masikitiko yangu kwa niaba ya MMK MEDIA GROUP wamiliki wa Swahili TV online, Swahili Radio Online na Blog ya Swahilitv.blogspot.com kuhusiana na yaliyojitokeza ubalozini."
Ni kweli kuwa nami niliyaona malalamiko hayo ambayo pia kwa kiasi fulani yalinisikitisha
Katika malalamiko hayo, MMK MEDIA iliandika kuwa "afisa huyu alikimbia vyombo vya habari rasmi na kualika video production company inayofanya shughuli za harusi kuwa mwakilishi wa Swahili Tv, Swahili Radio, Swahilitv Blog, na vyombo vingine vinavyoheshimika hapa DMV" (tazama screenshot hapa chini)
Hilo lilinisikitisha kwa kuwa NI DHAHIRI KUWA TUMEKUWA TUKIFANYA HABARI KABLA NA ZAIDI YA MMK MEDIA
Tumekuwa tukishirikiana HABARI (sio matukio na taswira tuu) na vyombo vingi vya habari nchini Tanzania KABLA YA KUZALIWA KWA MMK MEDIA.
Na katika hili, ushahidi upo wazi kwani sote tunaweka kazi zetu online, hivyo ni rahisi kwa wewe msomaji kuLINGANISHA UBORA WA HABARI katika KAZI ZETU ZA SAUTI (hapa) NA KAZI ZAO (hizi hapa) ama KAZI ZETU ZA VIDEO (hapa) na KAZI ZAO (hapa)
Kwa kumalizia tu, niseme kuwa SIPINGI HAKI YA MMK MEDIA KULALAMIKA, ila nasikitika kuwa WAMETUMIA BARUA YANGU BINAFSI KUJAZIA MALALAMIKO YAO HADHARANI, na pia wameshindwa kuwa wawazi kuhusu malalamiko yao ya awali ambayo kwa namna moja ama nyingine YALIPOTOSHA KUHUSU JAMII PRODUCTION NA KAZI ZAKE.
Lakini bado (BILA IDHINI) wametumia nakala ya barua yangu kutimiza lengo lao.
Katika hili nimesikitishwa na ningependa NILIWEKE HILO WAZI.
Mubelwa T Bandio
MTAYARISHAJI / MTANGAZAJI
JAMII PRODUCTION
Bofya soma zaidi upate Malalamiko ya MMK GROUP na Barua ya Mubelwa Bandio
JE! UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI UNABAGUA VYOMBO VYA HABARI AU AFISA HABARI WAKE NDIYE ANAYEBAGUA ?
Na Alex Kassuwi wa Swahili TV na Swahili Radio Online
Wiki iliyopita baada ya kulemewa na maswali kutoka kwa wasomaji,wasikilizaji, watazamaji na wafuatiliaji wa vyombo vyetu vya habari vya MMK MEDIA GROUP watu wengi sana walituuliza "kwa nini Swahili TV na Radio hawakuwepo katika tukio kubwa la kihistoria lililofanyika jumatano ya sept 18, 2013 katika ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani, ambapo Mabalozi wa Heshima (Honorary Consuls) walisaini mikataba mbele ya Rais wetu Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete.

UKWELI NI KWAMBA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI UNABAGUA VYOMBO VYA HABARI AU AFISA HABARI WAKE MINDI KASIGA
Baada ya tukio hafla hiyo kubwa kupita bila kusita niliandika masikitiko yangu kwa niaba ya MMK MEDIA GROUP wamiliki wa Swahili TV online, Swahili Radio Online na Blog hii ya Swahilitv.blogspot.com kuhusiana na yaliyojitokeza ubalozini.
Leo hii katika tahariri hii nitaelezea na kufafanua makosa yaliyofanywa na Ubalozi ama Mindi Kasiga na kwa nini hakupaswa ama hawakupaswa kubagua vyombo vya habari katika tukio lile.
PIA NIMEAMBATANISHA BARUA YA MAMALIKO TOKA KATIKA CHOMBO KINGINE CHA HABARI KWA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI.
PIA NIMEAMBATANISHA BARUA YA MAMALIKO TOKA KATIKA CHOMBO KINGINE CHA HABARI KWA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI.
HIVI NDIVYO WAANDISHI TULIVYOTENDWA
Mosi; Mindi alionyesha dharau kwa kuwasiliana na vyombo vya habari kwa ujumbe mfupi wa email kutokea kwenye iPad yake katika akaunti yake binafsi ya gmail na badala ya kuandika barua ya kiofisi yenye nembo husika na yenye kumbukumbu na sahihi husika kama ilivyo kawaida. Kuthibitisha kwamba ni dharau, Mindi Kasiga alionyesha heshima pekee kwa shirika la habari la kimarekani VOA (Voice of America) kwa kuwapelekea barua ya kiofisi ya kuwaalika rasmi iliyozingatia taratibu zote za na sheria za kiofisi.
Pili; Mindi alisingizia ufinyu wa nafasi kuwa mdogo kwa vyombo vingine vya habari na huku mwaliko wa VOA ukiwa wazi kwa idadi ya watu wowote wale watakaopenda na watakaotaka kuhudhuria hafla ile wote walikaribishwa bila masharti.
Tatu; Mindi hakupaswa kujiamulia kwa kusema namnukuu "upande wa electronic media wote mtawakilishwa na jamii production". Swali 1. kwa Mindi hivi unaelewa nini kuhusu electronic media? au bado umebaki na mtazamo wa zamani ambapo kulikuwa na print na electronic iliyomaanisha Radio na TV ambavyo vilikuwa analojia, na tena terrestrial zikirusha matangazo kwa minara na mikonga ya mawasiliano. Swali 2. je, vipi kuhusu digital media? blogs, Online TV, Online Radio na Websites? hujui kwamba ndio vyombo vya habari vya leo vyenye wasomaji na wafuatiliaji wengi? Swali 3. Ni Criteria gani Ubalozi ama Mindi Kasiga waliyotumia kuiteua Jamii Production kuwakilisha vyombo vingine vya habari katika tukio la Kitaifa?Nne; Mindi hukupaswa kuagiza vyombo vya habari vingine vipeleke maswali kwa Jamii production. Nakunukuu
"kama kuna maswali yaelekezwe kwao" Mindi huwezi kuagiza chombo cha habari kupeleka maswali yake kwa chombo kingine, kisha kile kingine kwenda kuuliza na kuleta majibu, hii haipo katika dunia ya sasa labda karne zilizopita. Jiulize ni kama vile Ikulu wana hafla halafu unaagiza TBC Taifa wapeleke maswali yao ITV halafu ITV wakaulize na kisha kuwaletea jibu TBC Taifa! uliona wapi hiyo?
BARUA YA MALALAMIKO TOKA KWA MWANDISHI MWINGINE AMBAYO ILITUMWA APRIL 2013 KWENDA UBALOZINI
Na Mubelwa Bandio
Shikamoo Mama Munanka.
Natumai kuwa u-mwema na unaendelea vema na kazi za kila siku hapo ofisini.
Binafsi ni mwema na naendelea na pilika za maisha hapa.
Napenda kutumia nafasi hii kueleza masikitiko yangu kidogo kuhusu hali ninayoona ikitokea kati ya ubalozi na jamii kwa ujumla.
Ntajaribu kufupisha jambo hili linalonisumbua sana
Nimekuwa mmoja wa wanaoletewa maswali ya “kwanini hamjazungumza na viongozi waliokuja hapo ubalozini” na kwangu nimepata wakati mgumu hata kufikiria jibu.
NI KWA KUWA HATA MIMI HUJIULIZA SWALI HILO
Nilishawahi kuleta maelezo na hata maoni ya namna ya kusaidiana na ubalozi kuunganisha jamii yetu hapa.
Binafsi naamini kuwa HAITATOKEA HATA SIKU MOJA, KUKAWA NA UJIO WA WAZIRI AMA RAIS AMA KIONGOZI YEYOTE WA NCHI KWA DHUMUNI MOJA TU LA KUKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI.
Ina maana, pale wanapopata ziara za kikazi, ndio wakati muafaka wa kukutana na / ama kuwasiliana nasi waTanzania tuishio huku (kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe.)
SOTE TUNAJUA HILI SI KAWAIDA
Nilipata kuleta WAZO hapo ubalozini kuwa inapotokea ikajulikana kuna Mheshimiwa anayekuja, waTanzania katika DIASPORA waelezwe na waweze kutuma maoni kwa mhusika wa habari hapo ubalozini (kwa njia ya barua pepe), na mheshimiwa akija, tujumuishe maswali ya wanaDIASPORA na yale yatakayoandaliwa na wadau wa habari na kufanya mazungumzo nao.
Hii ingekuwa NJIA RAHISI NA MUAFAKA ya kuwasilisha mawazo, maswali na hata dukuduku la mTanzania wa Marekani popote alipo.
Lakini badala yake, tumekuwa tukisikia kuwa “walikuwepo” na / ama kuwaona katika MATUKIO na kisha wanaondoka.
Katika hili, NAONA KAMA UBALOZI UMETUANGUSHA KATIKA KUTUUNGANISHA NA WALE WANAOTUONGOZA.
Naamini mjadala na kiongozi toka Tanzania (iwe ni Townhall meeting ama mahojiano yanayoratibiwa na ubalozi) ni muhimu kwa jamii yetu
Nina hakika kuwa mikutano ya viongozi wanaokuja wanapokutana na viongozi wa Jumuiya na / ama vyama haikidhi mahitaji ya waTanzania wote nchini kwa kuwa wanakutana na viongozi wa Metropolitan waliyopo nao hawakutani na wanachama wote (hata wenye nia).
Nimeona niwasilishe wazo langu hili kwa mara ya mwisho nikiamini kuwa utawekwa utaratibu muafaka wa kuTUMIA VEMA ZIARA HIZI kuweza “kuua ndege wawili kwa jiwe moja”
Yaani, ndani ya ziara zao za kikazi, waunganishwe nasi watanzania tulio huku.

Natanguliza shukrani
NB: Nimewaambatanisha wanahabari wenzangu wa hapa DMV.
Chanzo:www.changamotoyetu.blogspot.com
mwisho wa barua ya Bandio
NAMALIZIA KWA HILI MUHIMU
Pamoja na mamaliko ya Mwandishi mwenzetu Mubelwa Bandio bado Ubalozi au Afisa habari wake hawajajirekebisha na bado kero ziko palepale na vyombo vya habari.
Swali, kwa nini viongozi wa kiserikali wanapokuja katika ziara za kikazi hapa nchini Marekani Ubalozi hautoi taarifa kwa vyombo vya habari? na badala yake Ubalozi unatumia chanzo kimoja cha habari, ambapo mwanahabari mmoja huyo anatumika ku-brake news za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati sisi wanahabari wengine tunastukizwa na habari za ujio wa viongozi walifika lini, wamefanya nini nk toka katika chombo hiki kimoja na tunabaki tukijiuliza hiki ni chombo binafsi ama kitengo cha Ubalozi? Tungependa kuwe na Freedom of Speech, na Ushirikishwaji kwa vyombo vya habari vyote bila kubagua. Vyombo vya habari vipo na vinajulikana na Ubalozi unavitambua kwani vilishajitambulisha.

21 comments:
niliwahi ku-comment humu lakin mh dj luke kwasababu binafsi hukutoa my comments lakini niliyoyasema ndiyo yanajitokeza na aibu hii kwa nchi.
Narudia utaratibu wa kuwapata wafanyakazi ofisi za ubalozini hapo marekani na maybe kwingine utazamwe upya na Serikali lasivyo huko mbele mambo yatakuwa ya aibu sana na ajabu kubwa. Nilisema baada ya kuona pics uteuzi wa maofisa wa ubalozi marekani kuna walakini maana kila surname ni ya mkubwa fulani tz na sikuona hata jina moja la mtu aliyetoka familia isiyo na jina tz. I am sure kuna watu very competent wa familia za kawaida ambao wanaweza kufanya vizuri hapo ubalozini.
Hebu angalia email iliyotumwa jinsi ilivyo na typing&grammar errors..kweli hii inafaa kutumwa na mtu ambaye ana-status ya diplomat?kweli hii ndio competence level ya wa-tz?hatuna vijana competent kwa watu 45mil?aibu gani hii ndugu zangu??
Narudia tena Serikali yetu iangalie upya taratibu za ajira kwenye idara nyeti kama embassy na isifanye mchezo huu unaondelea maana madhara yake ni makubwa sana. Mh dj luke nina-andika kwa uchungu sana na mwelekeo wa nchi na nadhani pia wewe una jukumu la kusaidia katika hili
mdau
Denmark
I don't the whole story, but what I know the author of this article he either doesn't understand kusoma na kuandika au he is lacking of something.
Huwezi kusema nyinyi ni media wakati hamjui hata kuandika article.
Iddi
Ukweli uko palepale, mnaanzisha vyombo vya habari wakati hamna utaalamu. Shule hamtaki kwenda mnaanzisha kiholela habari. Mfano MMK hakuna la maana mnalofanya zaidi ya kujiwekea ujiko hamna jipya, na hata Aleex mwenyewe ni mbabaishaji, hivyo lazima muelewe mambo ya protokali na wageni wa heshima. Mahojiano yaSwahili na msiba wa uliotokea Howard University ulidhihirisha wazi kuwa si waandinshi ni wababaishaji. asante.
Ubalozini ubaguzi mwingi! Kwenye mialiko hata familia zao hatuzionagi
Kwa wafuatiliaji wa mambo na habari kwa ujumla data zinaonyesha wazi MMK ni washereheshaji wa harusi na debe na hawana ile taaluma, kwani hata mwakilishi wake hapa DMV ameonyesha hana taaluma yeyote ni ile jisifu, pata utaalamu sivyo basi kila mtu angeingia kwenye fani. ni swala la kununua vitendea kazi na kuomba leseni. Swala la Ubalozi lilifuata taratibu za kitaalamu hakuna sababu ya kulaumu. Msijilinganishe na VOA.
Waswahili wanasema mtaka cha uvunguni sharti ainame. Huwezi kuleta mabadiliko sehemu yoyote ukiwa nje ya ulingo. MMK msitumie mabavu kwa sababu haya mapungufu yapo kabla yenu msichukulie ni nyinyi tu mlibaguliwa. Tafuteni njia za mkato kuweza kuingia ubalozini, halafu mnaweza kupendekeza mabadiliko mkiwa ndani. Kumuandama Mindi sio tija hata akiondolewa taratibu zinabaki pale pale. Yeye ni mtu mdogo sana kufanya maamuzi tofauti na ubalozi unavyoendeshwa. Mtafuteni katibu mkuu wizara ya mambo ya nje atawapa muongozo woooote wa shughuli ubalozini. Wafanyakazi wake wanatekeleza tu.
Mdau,
Alexandria, Va
Kusoma na kuielewa fani kutasaidia sana, shule zimejaa bwelele hapa marekani lakini hamtaki kuwa proffessionals, hakuna sababu ya kubabaisha kabisa na mnaishi dunia ya kwanza kwenye resources za kutosha. Wabongo tuachane na mambo ya kuiga kila wakati jamani mtaiga vitu vingapi? Ni nani mwenye akili atawaita nyie kwenye shughuli kama vyombo vya habari kweli? MMK nadhani mnanisoma
Hizi blogs,online radios na TVs zimesajiliwa ? Ubalozi unafahamu kama hizo ni legal entities za tasnia ya habari kwa wana diaspora ? Rules,Regulations na guidelines za ubalozi zinasemaje juu nani aalikwe nani asialikwe ? Kwa criteria zipi ? Kama nyie wa huko DC mnalumbana kualikwa ubalozini,vipi juu ya news media zilizopo states nyengine ?
Tuliona picha kwenye globu ya Dj Luke,viongozi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi DMV walialikwa siku Rais Kikwete alipokuja.Mbona hatukuona wawakilishi wa CUF,CHADEMA na vyama vyengine ?
Hivi hawa mmk wamesomea hii fani au wanacheza manake baada ya kuangalia mahojiano ambayo wameyafanya mpaka sasa haihitaji kipofu wala kiziwi kujua hawa watu hawana hii taluma ingekuwa vyema wangefanya kitu ambacho wanaulevu nacho au waende shule kujifunza taaluma hii.
Ubalozi siyo kazi yake kuangalia masilahi ya economic refugee. You guys are crazy, u left the country but you still want to be looked after by the Embassy. Get real, ubalozi una kazi zake siyo kuwatumikia nyinyi. Endeni kwa Obama. Probably you are all USA citizens. Acheni ubalozi ufanye kazi zake za kibalozi. Who cares if you are invited. They can't invite every economic refugee.
Hahahahaha!!!! Katika kusoma comment zoote na kuzielewa, nimegundua kuwa there is a problem UBALOZINI hakikaa! Kuna baadhi ya vitu vya kurekebisha Kama usawa, ushirikiano baina ya waTZ walio USA na ubaloz.! Pia nimegundua walalamikaji wa MMK hawana uzoefu wa kutosha katika sector Yao ya utangazaji maana kuna comment Kama tatu au nne zimeeleza kuwa warudi shule kwa misaada wa utangazaji bora yaani wa Polish utangazaji na sio kuunga unga. Good luck to you all. MUNGU Ibariki Tanzania.
NDUGU ALEX, ni vizuri ukajifunza taratibu na sio kuropoka tu na kujiandikia utakavyo. Huna cha kumlaumu ofisa wa ubalozi kwa kazi usizozijua sawa sawa. Hii inadhihirisha wazi unavyotaka vijisifa na huku huna utaalamu wowote ule. Nani anahuo muda wa kukusikiliza kwenye redio mbao!!. Pole acha ubalozi ufanye kazi zake ipasavyo chini ya taratibu zake.
NINYI WASWAHILI MNAOJIITA MEDIA, MNAPOALIKWA UBALOZINI NI PREVILAGE TU. SIYO HAKI YENU KUPEWA MIALIKO YA KIOFISI. MSIJILINGANISHE NA VOA. HAMNA LESENI, HAMJASAJILIWA, HAMLIPI KODI, WALA HAMNA CERTIFICATE OF INSURANCE RIABILITY. UBALOZI UNAPOANDIKA MIALIKO UNATUNZA KUMBUKUMBU ZAKE. MIALIKO YA KIOFISI INATUMWA KWA WATU WANAOFANYA SHUGHULI ZA KIOFISI KISHERIA. KUBEBA VIDEO CAMERA SIYO HAKI YA KUMILIKI TV. FIGHTING FOR PREVILAGE IS LIKE BRINGING A KNIFE TO A GUN FIGHT. MLISOMEA SHULE GANI MAANA SIAMINI KAMA YOU ARE THE PRODUCT OF US EDUCATION. BADALA YA KULAIUMU UBALOZI NA MAAFISA WAKE NAWASHAURI MUENDE SHULE. MSIHARIBU UHUSIANO MZURI KATI YA JUMUIYA YETU NA UBALOZI WETU. NAOMBA MTOE LESENI ZA MEDIA ZENU NA KUOMBA SAMAHANI UBALOZI WETU MARAMOJA.
wewe unaesema ubalozi una kazi zake sio economic refugees blah blah I think huelewi kabisa unachoongea , kwanza kwa taarifa yako kazi moja kubwa sana ya ubalozi is" to cater for the Tanzanians living in that foreign country".Hata cater for the welfare of Tanzanians living abroad ni moja ya kazi za ubalozi... Wengi hapa sio citizens wa Marekani yet....One thing ni kwamba ubalozi unatakiwa kufanya kazi kwa usawa kwa watanzania wote.
Ni hilo tu,hayo mengine kwa leo nanyamaza.....lol
Ubalozi hautoi mualiko wa ki-ofisi kwa watu waoendesha biashara kinyume cha sharia. Kutoa video clips kwenye mitandao hakuna maana kuwa mnamiliki TV. Sisi tunavyojua ni kuwa lincesed TVs zinapatika local au cable. Ninyi mnapatikana channel gani?
Jamani ubalozini kuna nini kila tukio mnataka muwepo, kwa nini msitafute habari kwingine mpaka zitoke ubalozini. Ningewashauri muendelee na maisha yenu badala ya kung'ang'ania sehemu ambayo hamtakiwi. Wanaamini wao ndio watanzania halisi.
nikisoma haya majibizano na email ya ofisa ubalozi naungana na mdau wa kwanza kuwa wote hao media na huyo ofisa ubalozi UWEZO WAO na TAALUMA ZAO ni ndogo sana na wote wanatakiwa kwenda shule.
Embassy ni sehemu so serious na inahitaji wafanyakazi serious na haya ndio matokeo ya kuweka incompetent people maana real competent&professional asingeweza hata kualika kwa email hao wanaoitwa unprofessional media.
mdau
canada
Kueni wastarabu sote ni ndugu mnaoweka maoni yenu muhimu ni kutoa ushauri wako zaidi ili itilafu zetu ziondoke ila siku zote mchimba kisima ....... .......................................?
Wewe mdau wa saa 9.15pm,unachekesha sana eti hamjasajiliwa hamlipi kodi haohao wenyewe hapo baadhi ya wafanyakazi sio original kutoka bongo wamechopekwa tu hapa na hawalipi kodiiiiii wanatakiwa kuripoti wanachoearn huko IRS lakini hawafanyi na anoyn wa kwanza kabisa nakubaliana na wewe hao watu hapo utasikia oooh shangazi,mjomba shemeji yake alikua anafanya kazi hapa ndio maana wamemuajiri yaani ni upendeleo wa nguvu wa kindugu kuna,tabia hiyo naombeni muioache na kuna watu hapo hawajui hata kiingereza kabisaaaa mnatia aibu wageni wakija na ujeuri juu,fatilia kwa makini utaona asilimia kubwa wamechopekwa sio original diplomat from Tanzania,usibanie hii luka tafadhali.
Pitisha fagio la chuma ubalozini.
Post a Comment