Shirika la kimataifa linalohusika na kuangamiza silaha za kemikali nchini Syria, OPCW, linasema wataalamu wake wa kwanza watawasili Damascus Jumaane.
Shirika hilo linasema wakaguzi wake wana malengo matatu muhimu:
- kutathmini maeneo ya silaha za kemikali za serikali ya Syria.
- kuhakikisha silaha ambazo tayari zimefichuliwa na Rais Assad.
- kusaidia kuhakikisha shabaha ya kuangamiza hizo silaha itafikiwa.
Mpango wa Marekani na Urusi ni kuwa shehena hiyo ya silaha imalize kuangamizwa ifikapo kati ya mwaka ujao.
Lakini kuna sehemu kama 45 za kukaguliwa na kuna wasiwasi kuwa kazi haitamalizika kwa tarehe inayotarajiwa.
No comments:
Post a Comment