Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo ameshangazwa na hatua ya uongozi wa Shule ya Sekondari Hollywood ya Wilayani Mbozi kuwalazimisha wanafunzi kuvua viatu na kuviacha mlangoni wakati wanapoingia kwenye maktaba ya shule hiyo kwa ajili kujisomea, huku chumba cha maabara kikiwa ni kichafu na kilichojaa vumbi.
Mulugo alishuhudia tukio hilo juzi alipofanya ziara ya kushitukiza shuleni hapo na kuwakuta wanafunzi zaidi ya 20 wakiwa ndani ya chumba cha maktaba wakijisomea, huku wakiwa wamevua viatu na kuviacha mlangoni.
Mmoja wa walimu aliyekutwa ndani ya maktaba ambaye hakutaja jina lake, alisema wanafunzi hao hutakiwa kuvua viatu kwa sababu baadhi yao wamebainika huwa wanaiba vitabu vya shule na kuvificha kwenye viatu na kuondoka navyo.
“Tulibaini baadhi ya wanafunzi wakiingia maktaba na viatu wanaiba vitabu na kuvificha kwenye viatu na kuondoka navyo bila sisi kujua, hivyo tukaamua kuwa kila mwanafunzi anayeingia maktaba ni lazima avue viatu na kuviacha mlangoni,” alisema mwalimu huyo.
Hata hivyo, Mulugo alipinga vikali sababu hiyo akisema mwanafunzi anaweza kuiba kitabu na kukificha sehemu nyingine na akaondoka nacho bila ya walimu kujua.
“Hii siyo sababu ya msingi kwa sababu wizi ni tabia ya mtu, anaweza kuficha kitabu kwenye shati kwapani na bado akaondoka nacho bila ya ninyi kujua, hivyo sioni sababu ya msingi ya kuwavua wanafunzi viatu wanapoingia maabara na ninaagiza hili lisitishwe mara moja,” alisema Mulugo.
Naibu Waziri huyo wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, aliwataka walimu hao watafute mbinu nyingine ya kudhibiti wizi na siyo kuwazuia kuvaa viatu ndani ya maktaba.
Aliwatangazia wanafunzi wa shule hiyo kuwa amefuta mara moja utaratibu wa kuvua viatu wanapoingia ndani ya maktaba na kuwaeleza kuwa kuanzia sasa kila mwanafunzi anayekwenda kujisomea maktaba aingie akiwa amevaa viatu na kuwataka wajiepushe na wizi wa vitabu.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment