"TAARIFA YA MSIBA WA MWL. OSCKAR YAGAZA - KOROGWE TANGA
Familia ya Yagaza ya Korogwe, Tanga inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Mwl. Osckar Yagaza uliotokea siku ya Jumatatu, Oktoba 28, 2013. Shughuli za mazishi zitafanyika siku ya Alhamisi Novemba 7, 2013 nyumbani kwao Manundu Korogwe.
Wana-Yagaza USA watakuwa na mjumuiko wa sala ya Misa Takatifu kumuombea marehemu siku ya Ijumaa Novemba 1, 2013 saa 11 jioni nyumbani kwao 16 Robinson Street Binghamton, NY.
Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani, amina."
Asante sana kwa msaada wako, pamoja na ujumbe huu ninaambatanisha picha ya marehemu.
Kwa niaba ya familia ya Yagaza.
Elizabeth.
No comments:
Post a Comment