ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 22, 2013

HIZI NI SABABU TATU KUU KUHUSU ZITTO KABWE KUVULIWA NYADHIFA ZOTE CHADEMA.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemvua nyadhifa zote Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.

Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu wamepewa siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama.

4 comments:

Anonymous said...

CJUI CHADEMA INAELEKEA WAPI,KMELETA UPNZAN WA KWELI TZ SASA NAONA KNATAKA KUSAMBALATKA,2TAKOSA MUELEKEO KAMA MWANZO

Anonymous said...

CHADEMA NI CHAMA KIKUBWA TENA CHENYE UMRI MKUBWA TU (MIAKA 20 SI HABA)HIVYO KAMA TAASISI ILIYOKUA SI VIBAYA KUJITATHMINI NA KUREKEBISHA KASORO ZINAZOJITOKEZA. ZITTO ALIJITAHIDI KUWA MBALI NA KAZI ZA CHAMA CHAKE KIASI KWAMBA SISI TULIO NJE YA CHAMA HICHO TUKAHISI ZITT0 NI "CEREMONIAL LEADER" NA HANA KAZI ZA KUFANYA NDANI YA CHADEMA. TULITARAJIA KWA MFANO AISAIDIE CHADEMA AKIWA KAMA NAIBU KATIBU MKUU KUPAMBANA NA HOJA/KAULI CHAFU/TATA ZA MWIGULU NCHEMBA (NAIBU KATIBU MKUU WA CCM) LAKINI HILO ZITTO HAKUFANYA HATA SIKU MOJA KWA MIAKA YOTE YA UONGOZI WAKE KATIKA WADHIFA HUO...NAFIKIRI CHADEMA WAMEFANYA UAMUZI MGUMU NA UNAWEZA KUWASAIDIA ZAIDI KULIKO KUWASAMBARATISHA...CHADEMA KINAHITAJI NGUVU YA UONGOZI WA PAMOJA WENYE KAULI MOJA AU YA PAMOJA WANAPOWASILIANA UMMA MKUBWA WA WANACHADEMA, WAPENZI WA CHADEMA, MASHABIKI WA CHADEMA NA WANANCHI KWA UJUMLA...ZITTO AJISAHIHISHE ILI AKUBALIKE KWA UMMA HUO MKUBWA NA PIA KUISAIDIA CHADEMA ILI ISONGE MBELE NA AEPUKE KUWA ''RETARDING FORCE'' KWA KUHUJUMU KWA NAMNA YEYOTE ILE OPERESHENI NA MIKAKATI YA CHAMA CHAKE...MUNGU IBARIKI TANZANIA...MUNGU YABARIKI MAGEUZI YA KISIASA TANZANIA YALETE TIJA KWA TAIFA LEO NA SIKU ZOTE ZIJAZO.

Anonymous said...

mimi nafikiri huyo jamaa hapo juu ni gamba, hajui ili chama au kiongozi uendelee kukubalika na jamii huna budi kufanya maamuzi magumu kama haya ili kuepuka watu wasiokitakia mema chadema

Anonymous said...

NA NYIE ACHENI USHABIKI KWENYE MAMBO MAZITO KAMA HAYA YALIYOTOKEA WE JENGA HOJA USIMSHAMBULIE MWENZAKO. UKWELI NI KWAMBA CHADEMA INAELEKEA KUFA KUTOKANA NA HISIA ZA KILAFI ZA KINA DR.SLAA NA MWENZAKE MBOWE HALAFU MNAJIFANYA VIPOFU HAMUONI? MBONA WASIOKUA NA MADHARA KAMA KINA MACHEMLI, SUZAN LYIMO NA WENGINE WASIOKUA NA MUELEKEO WA KUGOMBEA CHEO CHOCHOTE HAWASUMBULIWI WALA KUJADIRIWA? U DEMOKRASIA WENU UPO WAPI SASA? MMEKUA CHAMA CHA HAWAAMBILIKI SASA HIVI.