ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 2, 2013

Kutana na pichaz za Poetry Addiction ya @FidQ jana, alichosema kuhusu muziki ulichomfanyia kiuchumi mwaka 2013



Hii Poetry Addiction au Uaraibu wa Mashairi ni event inayoandaliwa na rapper Fid Q na timu yake ambapo hii ya jana November 1 ilikua ya tatu kufanyika na ikashirikisha vipaji vya kike peke yake.

Kwenye Exclusive interview na millardayo.com rapper Fid Q amesema muziki ulichomfanyia kiuchumi mwaka huu ni pamoja na kumsaidia kufanya project zake mwenyewe bila kusubiri au kutegemea wadhamini.
Anasema ‘tangu zamani nilikua na idea ya kufanya vitu vingi sana lakini unapeleka wazo kwa mdhamini anachomoa… mwaka huu nilipata akili mpya ya kuchanga kila sumni ninayopata na ninapotaka kufanya kitu changu nakifanya kwa kujisachi mwenyewe mfukoni, kama hii Poetry Addiction sina mdhamini lakini naweza kuleta wasanii kutoka nje nawalipia ndege, hoteli na mengine kwa hela yangu… atleast mwaka huu nimeuona mtaji naweza kufanya vitu vyangu ninavyotaka mwenyewe’

Fareed Kubanda anasema ‘ninasikitika sana kukutaarifu bwana Millard kwamba hawa watu wa masoko kwenye makampuni makubwa wengi wamekua wanafiki, wamekua wepesi kutoa pesa nyingi kwa wasanii wa nje lakini hawako tayari kuwapa wasanii wa hapa, silalamiki kama mjinga… nalalamika kama Mtanzania ambae anasisitiza uzalendo, sizungumzii Mapromota.. nazungumzia hawa watu wa marketing wakipelekewa proposal wanasema umetuwekea huyu wa nje hapo safi ila huyu mwingine si mbongo tu?!

‘Nilikua naomba watu wa Marketing kwenye makampuni ya Tanzania waache uzandiki na wasupport wasanii wetu, waache ukiritimba kuona wasanii wa bongo hawastahili kulipwa sana ndio maana wasanii kila siku wanaota, wanaamua kujizushia tu kwamba wamefanya video za milioni 30 lakini ukiangalia video yenyewe hata milioni 10 haijatumika, na ni vigumu kwa wasanii wetu kufikia hizo levo kwa sababu watu wanaungaunga, hela hiyo hawana.. wajaribu kuwatengenezea mazingira basi’ – Fid Q

No comments: