ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 2, 2013

MALINDI CLUB MOSHI YAJAA VIBAKA WAKATI WA USIKU

kwa wale wanapendelea kutembelea malindi club iliyopo moshi mjini wakati wa usiku nawapa tahadhari wakati wanapokuja na magari yao waakikishe yanausalama wa kutosha kwasababu sasa hivi malindi club sio salama kuna vibaka wengi na machangudoa wanaoshirikiana na hao vibaka kufanya udokozi wa mali za watu katika magari na pia muwe na tahadhari mnapokodisha bodaboda zinazopaki malindi wakati wa usiku kwasababu wengi wa madereva wa bodaboda katika club hiyo ya malindi ni vibaka ukimkodisha anakupeleka anakufikisha mahali na kukunyang'anya kila ulichonacho.

MACHANGUDOA

hivi jeshi la polisi, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa manispaa ya moshi mjini mpo wapi? nashangaa malindi club na hii barabara ya kupandisha mpaka kanisa la kristo mfalme limejaa machangudoa na vijana wengi sijui na wao ni madalali wa kuwatafutia wateja awa wadada wanaojiuza usiku?mimi sijui sheria naomba kuuliza hivi Tanzania hakuna sheria inayokataza biashara ya ukahaba au amani yetu tuliyo nayo hapa nchini ina mruhusu mtu kufanya hii biashara? mimi naangalia kama awa wafanya biashara wanaojitafutia pesa kwa kuuza bidhaa labda unakuta wamepanga kando ya barabara utakuta wanachukuliwa hatua kali lakini awa wafanyao biashara ya kuuza miili yao hakuna wanalofanywa.

No comments: