Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi wa CCM wilaya ya Namtumbo mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mchomoro ,wilaya ya Namtumbo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa wakati wa mapokezi katika kijiji cha Mchomoro wilaya ya Namtumbo.
Wakazi wa kijiji cha Mchomoro wakiwa wamejipanga kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake.
Mbunge wa Namtumbo Ndugu Vita Kawawa akihutubia wananchi wa Mchomoro ambapo alisema waziwazi Vyama Vya Msingi vya Ushirika haviwasaidii wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mchomoro wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Balozi wa Nyumba Kumi Ndugu Said Hussein akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye shina lake namba 6 katika kijiji cha Mchomoro wilaya ya Namtumbo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa chai pamoja na Balozi wa Shina namba 6 Ndugu Said Hussein na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Ndugu Vita Kawawa.
Nchi inajengwa na wachaoakazi na viongozi mahiri ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishiriki ujenzi wa wodi ya wazazi ya Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tanesco kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Namtumbo.
Mbunge wa Namtumbo Ndugu Vita Kawawa akihutubia wananchi wa Wilaya ya Namtumbo kwenye Uwanja wa Taifa wilayani hapo na kutamka wazi wazi kuhusu watendaji wa vyama vya ushirika wanavyowaibia wakulima na kutaka Serikali kuchukua hatua mara moja.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Namtumbo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Madereva wa Bodaboda wa wilaya ya Namtumbo baada ya kufungua shina la CCM la Bodaboda wa Namtumbo.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akihutubia wananchi wa wilaya ya Namtumbo katika uwanja wa Taifa na kuwaambia wakina mama wagombee nafasi mbalimbali za uongozi na kutaka juhudi ziongezeke katika kusomesha watoto wa kike.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Namtumbo na kuwaambia moja ya jukumu la CCM ni kuwatetea wakulima na kutaka Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Chakula itatue masuala ya wakulima mara moja ili kuondoa kero zao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Namtumbo mkoani Ruvuma kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa wilayani hapo.















No comments:
Post a Comment