ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 21, 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Tishio la kukua kwa taka za elektroniki duniani

Photo credits:newswatch.nationalgeographic.com
Moja ya FAIDA zinazooenakana kuletwa na ndugu, jamaa na marafiki walio nje ya nchi ni pamoja vifaa kama simu, tarakilishi (kompyuta) na vingine vya alektroniki ambavyo kwa wengine ni kigezo cha maendeleo ama kuendana na maisha ya kisasa
Lakini vifaa hivyo ambavyo vinaanza kuwa tishio la mazingira duniani kutokana na TAKATAKA zinazotokana na vifaa na bidhaa zinazoendana nazo. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa hivi karibuni, masalia ya vifaa hivi vya elektroniki inategemewa kukua kwa asilimia 33 kwa miaka mine ijayo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, uzito wa vifaa vya elektroniki pamoja na majokofu inategemewa kuongezeka kutoka tani milioni 48.9 mwaka 2012 mpaka tani milioni 65.4 mwaka 2017.
Uzito huu ni sawa na uzito wa mapiramidi 11 ya Misri

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

No comments: