Bondia japhet kaseba wa daresalaam na alibaba Ramadhani wa Arusha wamemaliza zoezi la upimaji salama huku japhet akipata 79kgs na alibaba akipata 78kgs hivo wanaweza kucheza bila matatizo na mabondia wanaocheza katika utangulizi wote wapo katika hali nzuri .Pambano hilo litapigwa kesho katika ukumbi wa friends corner manzese kuanzia saa kumi jioni, pambano hilo lililoandaliwa na Ibrahim kamwe wa bigright promotion pia litawakutanisha mabondia zumba kukwe wa kibaha na Jacob maganga wa Tanga,lusekelo daudi na mbaruku heri,issa omar na moro best, mwinyi mzengela na shaban bodykitongoji.harman Richard na Adam yahaya,, shughuli za ndani ya ukumbi na ulinzi zitashughulikiwa na kiwango security na jeshi la polisi hivyo pambano litakuwa katika hali ya usalama zaidi
No comments:
Post a Comment