ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 21, 2013

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA SIKU YA JANA

Vijana wa UVCCM mkoa wa Iringa na Mbeya wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emanuel Mteming'ombe siku ya jana wakati wa kuelekea kanisani kwa ibada kabla ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini Kwake Rujewa Mbarali mkoani Mbeya.
Naibu katibu mkuu wa CCM Bara Bw Mwigulu Nchemba wa pili kulia akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu (kulia) na viongozi wengine nyumbani kwa marehemu Mteming'ombe Rujewa Mbarali.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro wa pili kushoto akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma (katikati).
kwa picha zaidi bofya zaidi
Familia ya marehemu na ndugu mbali mbali wakiwa kanisani kanisa la RC Rujewa siku ya jana.
Waombolezaji wakiwa ibadani siku ya jana.
Waombolezaji wakikimbia mvua kubwa iliyonyesha kwa dakika kama 10 hivi mara baada ya mwili kufika makaburini siku ya jana.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akisoma historia ya marehemu Mteming'ombe huku naibu katibu mkuu CCM Bara Bw Nchemba (kulia) akionyesha kufuta machozi.
Mjane wa Mteming'ombe akiweka maua.
Mzee Mteming'ombe akiweka shada la maua.
Naibu katibu mkuu CCM Bara Mgulu Nchemba akiongoza waombolezaji kuweka shaba la maua katika kaburi la aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa marehemu Emanuel Mteming'ombe siku ya jana katika makaburi ya RC Rujewa Mbarali Mbeya.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro akiweka shada la maua.HABARI NA PICHA NA FRANCIS GODWIN, IRINGA

No comments: