ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 19, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AELEKEA NCHINI MAREKANI KUFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA YAKE.


 Rais Jakaya Kikwete

 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA  
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini jioni ya jana, Jumatano, Desemba 18, 2013, kwenda Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za uchunguzi wa afya yake na kwa kutilia maanani siku za kusafiri kwenda Marekani na kurudi nchini, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini Alhamisi ya wiki ijayo, Desemba 26, 2013.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2013

8 comments:

Anonymous said...

Kwanini tu mh rais asichunguzwe na madaktari bingwa hapo muhimbili. Marekani hakuna mdaktari bingwa, kina ma-specialist tu. Yani anawaacha mabingwa na kwenda kutibiwa na wale wasiokuwa mabingwa. Wadau hii imekaaje?

Anonymous said...

Is that true, hard to believe. So basically there are no medical facilities in Bongo to even do a medical check up - what does it involve. I will do mine at Amana hospital and see how I go. Hongera JK, USA today where next after new year?

Anonymous said...

may be the local doctors and specialists are not well trained

Anonymous said...

Kwani hawezi kutibiwa nchini kwake? Wajifunze kuboresha idara ya afya ili wote tuwe tunatibiwa nyumbani, je wale wasio na uwezo waende wapi???

Anonymous said...

Hivi huyu rais amekaa nchini kwake japo 1 week akatenda kazi kwa wananchi? Come on jamani it's just too much!!!

Anonymous said...

Kwanini asiende Muhimbili?

Anonymous said...

Marekani dunia ingine! Huduma ziko juu, pia gharama zake sio mchezo. South Africa au India ghaama nafuu kidogo. Kurelax pia ni afya.

Anonymous said...

I wish you all the best uncle may God be with you and we will pray for you