ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 21, 2013

SHUKURANI ZA DHATI


Wafiwa katika picha kutoka kushoto ni Rehema (mke wa Nambay ) Nambay na Sackstus Kaitaba ndugu wa marehemu wakiwa kwenye harmbee iliyofanyika College Park Maryland

Familia ya Mosha inapenda kuwashukuru watu wote ukiwemo Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa msaada wa hali na mali na hatimaye kuwezesha kumsafirisha mpndwa wetu Mzee Maurice Mosha (baba yake Nambay) kwa mazishi nyumbani Tanzania. Mwili wa marehemu uliondoka Siku ya Ijumaa Dec 20, 2013 kuotokea Minnesota,

Jumla ya michango iliyokusanywa kutoka kwa watu mbalimbali ndani na nje ya Marekani ilikuwa $11,670, tunashukuru sana na hatuna cha kuwalipa kitakacholingana na moyo wa upendo mliotuonyesha katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa baba yetu na hatimaye kufanikisha na kuwezesha kumsafirisha baba yetu kwenda nyumbani Tanzania kwa mapumziko kwenye nyumba yake ya milele. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awazidishie saba mara sabini.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

No comments: