Mchezaji wa Kimataifa Emmanuel Okwi (kulia) akijumuika na wachezaji wenzake wa Yanga katika mazoezi yao yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kijitonyama leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa 'Nani Mtani Jembe' dhidi yao na Simba unaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Okwi amewasili jana jioni na kupokelewa kifalme na mashabiki wa Yanga hadi Klabuni mitaa ya Jangwani na kutambulishwa kwa mashabiki na kisha leo kujumuika na wenzake katika mazoezi ya pamoja.
Emmanuel Okwi (katikati) akiwa na wachezaji wenzake katika mazoezi ya pamoja kwenye Uwanja wa Kijitonyama, leo asubuhi.
Mazoezi yakiendelea.
Wachezaji wakipata maji baada ya mazoezi...
Okwi akizungumza jambo na kocha mkuu wa Yanga Brants.
Sehemu tu ya mashabiki wa soka waliofurika kwenye uwanja wa Kijitonyama kumshuhudia Okwi.
Hapa ni wakati wa mapokezi ya Okwi jana jioni alipowasili Bongo, akiongozana na baadhi ya viongozi wa Yanga.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga waliofurika kwenye Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jana kumpokea Okwi.
Foleni kubwa iliyosababishwa na msafara wa Okwi wakati wa mapokezi yake jana.
Msafara wa Okwi ukukatiza mitaani kuelekea Klabuni Jangwani.
Wa Boda boda nao walikuwepo kumpokea Okwi
Mashabiki wakiizingira gari iliyokuwa imembeba Okwi baada ya kuwasili Klabuni jana.
Okwi akipokelewa Jangwani
Sehemu ya mashabiki wa Yanga waliojitokea Klabu ya Yanga jana jioni kumpokea Okwi.
Okwi akinyoosha mikono kusalimia mashabiki. Credit:Sufiani mafoto
No comments:
Post a Comment