ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 12, 2014

MAZISHI YA MPENDWA WETU ZAINAB BUZOHERA AZIKWA LEO MAKABURI YA UKONGA

Mume wa marehemu Dullah (Tshirt nyeusi mbele ya kamera) akiwasili makaburini kwa mazishi ya Zainab Buzohera yaliyofanyika leo Jumapili Jan 12, 2014 Tanzania kaika makaburi ya Ukonga, Dar es Salaam, Tanzania marehemu alizikwa saa 10 jioni kwa saa za Tanzania hapa ilikuwa saa 2 asubuhi (8am ET)
Juu na chini ni Ndugu, jamaa na marafiki wakijiandaa kuutoa mwili wa mpendwa wetu tayari kwa mazishi yake yalioyofanyika leo Jumapili Jan 12, 2014 Ukonga, Dar es Salaam, Tanzania.
Mwili wa mpendwa wetu ukitolewa kwenye gari lililoubeba kuelekea makaburi ya Ukonga kwa mazishi.
Mosi akisaidia kubeba jeneza lililobeba mwili wa marehemu Zainab Buzohera mara tu ndugu, jamaa na marafiki walipojumuika na familia kwenye mazishi ya mpendwa wetu katika makaburi ya Ukonga, Dar leo. Mosi alishawahiishi DMV miaka ya nyuma.
Kushoto ni baba wa Zainab Mzee Buzo akiwa na ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye maziko ya mpendwa manae
Maziko yakiendelea.
Mume wa marehemu Dullah (Tshirt nyeusi anayefuta mkono na kitambaa) akifuatilia mazishi ya mpendwa mke wake.
Ndugu, jamaa na marafiki wakifanya sala.
kutoka kushoto ni Stephano Mhina, Milanga na Saleh Londa wote walishawahi ishi DMV japo Mhina yupo Tanzania kikazi.
 Watatu toka kushoto ni Yassin Njayaga ambaye alishawahi kuwa Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
kwa picha zaidi za mazishi na msiba nyumbani bofya soma zaidi

Umati wa watu waliojumuika pamoja na familia kumzika mpendwa wetu Zainab Buzohera aliyezikwa leo Jumapili Jan 12, 2014 mida ya saa 10 jioni kwa saa za Tanzania hapa ilikuwa saa 2 asubuhi (8am ET)katika makaburi ya Ukonga.
Ndugu, jamaa na marafiki waliofika nyumbani wakiingiza mwili wa marehemu kwenye gari lililobeba mwili wa mpedwa wetu kuelekea makaburi ya Ukonga kwa shughli za mazishi yaliyofanyika leo Jumapili Jan 12, 2014. Mwili wa marehemu uliwasili Tanzania siku ya Jumamosi Jan 11, 2014.
Juu na chini gari lililobeba mwili wa Zainab kwa safari yake ya mwisho.
Mama wa Zainab(gauni jeupe kilemba cheusi) akiwa mwenye huzuni huku akilia kwa uchungu wakati mwili wa Mpendwa mwanae ulipokua ukiingizwa kwenye gari tayari kwenda kwenye maziko yaliyofanyika leo Jumapili Jan 12, 2014 katika makaburi ya Ukonga mida ya saa 10 jioni kwa saa za Tanzania hapa ilikuwa saa 2 asubuhi (8am ET).
Wadau kutoka Marekani na wengine ambao waliwahi kuishi Marekani wakijumuika na familia katika mazishi ya Zainab ambaye amezikwa leo Jumapili katika makaburi ya Ukonga kwenye picha wa kwanza kushoto ni Saleh Londa, watatu toka kushoto ni George Mwaswaliba, watano toka kushoto ni Baraka Kifaru, wasita toka kushoto ni Stephano Mhina, wapili toka kulia ni Mosi na kulia ni Mussa mkaazi wa New Jersey.
Juu na chini kulia picha juu ni mume wa aliyekuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Shariff Maajar na aliyekaa kwenye kiti picha chini ni aliyekuwa mwambata wa jeshi Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Maganga wote kwa pamoja wakijumuika na familia kwa maziko ya mpendwa wetu Zainab Buzohera aliyezikwa leo Jumapili Jan 12, 2014 Tanzania katika makaburi ya Ukonga.
Msafara wa kuelekea mazikoni
Ndugu, jamaa na marafiki wakielekea mazikoni.

3 comments:

Anonymous said...

May her gentle loving and caring soul rest in peace. Gone way too soon my love. You'll deeply be missed by everybody. I had never met her but as a human being I was so touched by her sudden death. May God almighty give strength to the loved ones left behind. I know she's in a better place now.

Anonymous said...

Jamani Zainab tumekulilia wengi mpenwa wetu. Kwa kweli mazishi yako ni ya kukumbuka yaani yanaushirikiano. Kila mmoja ameshiriki jamani. Na mimi naomba siku yangu ikifika nizikwe kama wewe. R.I.P dear love

Anonymous said...

Mungu akulaze mahali pema Zainab; upendo wako na ucheshi wako ni vitu tutavikumbuka daima; Mola wape faraja wafiwa. Dulla mdogo wangu tukisema tutakufuru Mungu tunajua Zainab alikuwa ni mtu muhimu kwenye maisha yako Mola akupe maghufira!