Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na usalama, wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Amani, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, mjini yaliyofanyika leo.
Viongozi wa Serikali na viongozi waalikwa, wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akipunga mkono kusalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Amani katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo mchana
Sehemu ya watu wa liohudhuria sherehe.
Askari wa zamani wanaoigiza gwaride la enzi za ukoloni, 'Tarabush' wakipita mbele ya jukwaa kuu na kuonyesha jinsi askari hao walivyokuwa wakicheza gwaride hilo, wakati waa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na baadhi ya viongozi waalikwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, wakati alipokuwa akiwasili uwanja wa Amani leo mchana.
Viongozi wa Serikali na viongozi waalikwa, wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akikagua gwaride maalum la sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo mchana
Jeshi la JWTZ
Kikundi cha Halaiki
Maandamano ya wananchi
1 comment:
Zanzibar muungano unawarudisha nyuma.
Post a Comment