Na Mwandishi Wetu, Dodoma
CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM), kimesema kuwa hakitishwi na tambo la vyama vya upinzani
kuhusu hatua yao ya kwenda kushitaki kwa wananchi juu ya muundo wa
Serikali mbili.
Tamko
hilo la CCM limekuja siku chache baada ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kutangaza uamuzi wake wa kwenda kushitakiwa kwa
wananchi ikiwa msimamo wa CCM wa Serikali mbili utapitishwa katika
Bunge
la Katiba.
Alisema CCM haitishiki na wanaotaka kwenda kushitaki kwa wananchi kuhusu msimamo wao wa kutaka kuwepo kwa Serikali mbili.
“Wanaotaka
kwenda kushtaki kwa wananchi waende tutawafuata nyuma na majibu, hii
habari ya kutishiana tutaenda kwa wananchi kwani mwananchi huyo ni nani.
“Kama
wao wanauwezo wa kufika kwao na kujenga hoja na sisi tunao uwezo wa
kufika kwao na kujenga hoja, nasema watangulie kwa wananchi tutawakuta
huko na tutatoa majibu na wananchi watatuelewa.
“Kama
ambavyo wamekuwa wakituelewa kwa kipindi cha miaka 50, wanatuamini
tuendeele kuongoza nchi hii ndivyo watatuelewa katika suala la katiba,
“Tusifike mahali pa kutishia, tusifike mahali pakutaka kuburuzana sio sawa ni akili ni akili finyu,” alisema Nape
Akizungumzia
kikao hicho cha NEC kilichomalizika juzi, Nape alisema kilikuwa na
ajenda moja tu ya kujadili rasimu ya pili ya katiba na kwamba rasimu
hiyo ilijadiliwa kifungu kwa kifungu.
Alisema
pamoja na mambo mengine msimamo wa CCM bado ni uleule wa Serikali mbili
na kwamba walichojadili ni maboresho ambayo yanahitajika katika mfumo
huo.
“Mapendekezo
yetu ni kuwepo kwa Serikali mbili zilizofanyiwa maboresho ambayo ndiyo
yatajibu changamoto za mfumo huu kwa sasa na mapendekezo yetu
tutayasilisha kwa wabunge wa Bunge la Katiba,” alisema Nape
Alitaka
vyama vingine visiweke mazingira ya ugomvi kutokana na msimamo huo wa
CCM bali wajenge hoja zao kwa kile wanachokisimamia.
“Kila
watu wanamaoni yao wala sio ugomvi, watu washindane kwa hoja na hakuna
suala la nani kashinda au nani kashindwa,” alisema Nape
1 comment:
Bwana Nape anapaswa kutambua kuwa mjadala wa katiba si uchaguzi wa udiwani au mwenyekiti wa mtaa ambao mara zote hutawaliwa na ubabe & nguvu za misuli kuliko hoja za msingi.
CCM wekeni hoja za msingi wananchi wawaungeni mkono..
Post a Comment