Mabondia Thomas mashali na Japhet kaseba wamesaini makubaliano ya kucheza pambano la ubingwa wa mabaara wa Universal Boxing Organization (UBO) pambano litakalopigwa tarehe 29 march 2014 katika ukumbi wa karume hall zamani ukiitwa PTA hall. Pambano hilo linaandaliwa na mratibu mashuhuri katika masuala ya ngumi za kulipwa nchini hususani pande za Tanga Ally mwanzoa alifurahishwa sana kwa nidhamu iliyooneshwa na mabondia hao wakati wa zoezi la kusaini mkataba wa makubaliano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa vijana hall kinondoni yakishuhudiwa na viongozi wa ngumi na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari kiongozi wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim kamwe aliyefatana na Anthony ruta amesema makubaliano yamekwenda vizuri na wote wametia saini kupigana pambano hilo litakalopigwa katika uzani wa kilogram 79 na wamechukua malipo yao ya awali kuashiria kuwa pambano hilo lipo na kila mmoja amejigamba kumchakaza mwenzake siku hiyo na kujitengenezea mazingira mazuri katika ubingwa wake huo.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
No comments:
Post a Comment