Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ifunda kwenye kiwanja cha Ifunda Sokoni ambapo moja ya vitu alivyosisitza ni viongozi kuahidi ahadi zinazotekelezeka .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ifunda kwenye viwanja vya sokoni Ifunda ambayo alisema alikuja kuwajulia hali maana ni mwezi sasa tangia wamempoteza Mbunge wao Marehemu William Mgimwa na kwa vile alikuwa Mbeya kwenye maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM ,Katibu Mkuu akaona ni vyema kuja kuwasabahi na kuwapa pole wananchi wa jimbo la Kalenga.
Msanii wa kujitegemea Catherine Mzokolo akiimba wimbo unaoitwa CCM Nakupenda kwenye viwanja vya sokoni Ifunda wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akihutubia wakazi wa ifunda kwenye viwanja vya Ifunda Sokoni na kuwaambia kuwa CCM imejipanga madhubuti katika kudumisha umoja na mshikamano.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Dada wa Marehemu Dk.William Mgimwa nyumbani kwao kijiji cha Magunga kata ya Maboga mkoani Iringa,Katibu Mkuu alipita kuwajulia hali na kuwapa pole .
No comments:
Post a Comment