ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 3, 2014

MAMIA WAMZIKA MEJA MSTAAFU SAMWEL ISAAC CHEKINGO KWENYE MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR‏

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakibeba mwili wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Kinondoni kwa ajili ya ibada maalum.
Marafiki wa karibu wa familia ya marehemu wakiwa wamesimama kuupoke mwili wa marehemu Meja Mstaafu Isaac Chekingo ulipowasili nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa Juma.
Mtoto mkubwa wa marehemu (mwenye koti la suti jeusi) akijadiliana jambo na baadhi ya wanakamati wa msiba ulioongozwa na Afande Thomas Ndonde wa JWTZ.
Baadhi ya waombolezaji wakitoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo.
Baadhi ya watoto wa marehemu na wake zao wakiwa kwenye majonzi mazito.
kwa pcha zaidi bofya soma zaidi
Mtoto mkubwa wa marehemu Samson Samwel Chekingo (mwenye miwani) akijadiliana jambo na wadogo zake kabla kuanza kwa misa ya kumwombea marehemu baba yao.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Isaac Chekingo mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha (katikati) akiwa amejumuika na baadhi ya waombolezaji kwenye msiba wa Marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamefurika nyumbani kwa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
Mchungaji Charles Mzinga kutoka Kanisa la Usharika wa Azania Front akiendesha ibada ya misa ya kumwombea marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa juma.
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha akijumuika na waombolezaji wengine kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo.
Waombolezaji wakiendelea kutoa heshima za mwisho.
Pichani juu na chini ni watoto wa marehemu Meja Mstaafu Samwel Chekingo wakitoa heshima za mwisho kabla ya kuelekea makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya mazishi.
Vilio na simanzi vilitawala.
Mke wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa mpendwa mume wake.
Pichani juu na chini Familia ya marehemu ikiwa katika makaburi ya Kinondoni tayari kuanza shughuli za mazishi.

WASIFU WA MAREHEMU MEJA SAMUEL ISAAC CHEKINGO.

Marehemu alizaliwa tarehe 06.06.1953, alizaliwa Ng’ang’ange, Dabaga na alikulia Mufindi kibaoni – Mgelukwa.

Alisoma shule ya msingi Mufindi na shule ya sekondari Kigonsela.

Baada ya hapo alijiunga na Jeshi la Ulinzi wa Tanzania, na alihudhuria kozi mbalimbali za kijeshi, zaujuzi na uongozi. Pia kozi na kozi ya taaluma ya urubani nchini Canada.

Marehemu alitunukiwa medali mbalimbali za kijeshi zikiwemo:-

a) Medali za Ushindi.

b) MedaliVita ya Kagera.

c) Medali ya Miaka Miaka Ishirini ya Utumishi.

d) Utumishi wa Muda Mrefu.

Marehemu alishikizwa (Seconded) kwenye wakala wa ndege za serikali hadi alipo staafu jeshi akiwa na cheo cha Meja December mwaka 2000.

Marehemu akiwa Rubani wa ndege alipata nafasi ya kuwarusha viongozi mashuhuri kama:-

i) Marehemu Mwal. Julius K. Nyerere.

ii) Marehemu Nelson Mandela.

iii) Marehemu Pope John Paul II.

iv) Raisi Mstaafu Alhaji Alhasan Mwinyi

v) Raisi Mstaafu Benjamin W. Mkapa

Na viongozi wengine wengi wa kitaifa na wakimataifa.

Marehemu alipata fursa ya kushikizwa katika kampuni ya Williamson Diamond kama Rubani, pia Kahama Mining na baadae alifanya kazi nje ya nchi Darfur, Sudan na DR Congo.

Marehemu katika siku zake za mwisho alifanya kazi katika shirika la Air Tanzania hadi mauti yalipo mkuta.

Marehemu alianza kuugua mwanzoni mwa mwezi Januari, 2014 na alitibiwa katika hospitali mbalimbali hadi mauti yalipo mkuta tarehe January 28 ya mwaka 2014.

Marehemu ameacha mke na Watoto wa kiume wane na Watoto wa kike wawili.

SHUKURANI.

Mahospitali – regency hospital, Madakitari na wauguzi hasa Dr. Alfonsi, Dr. Kisanga, na madakitari wa hospitali ya jeshi Lugalo.

Uongozi wa ATC

Uongozi wa Jeshi la wananchi wa Tanzania walioridhia marehem kuzikwa kwa Heshima za kijeshi, maafisa na maaskari walioshiriki katika paredi za Mazishi, ndugu jamaa na marafiki walioshiriki kwa hali na mali kufanikisha katika kumpumzisha baba yetu mpendwa .

No comments: