Kwasasa Uganda, imekua nchi ya kuigwa kwa jambo jema,
nchi hiyo imepiga marufuku Vazi la “KIMINI” yani Nguo Fupi kwa wanawake wote
nchini humo.......
Taarifa hiyo imetoka mara baada ya Rais Yoweri
Museveni, kusaini mswada huo na kuwa sheria ya nchi, inadaiwa kuwa kuzuia
mavazi hayo kutasaidia sana
kupunguza vitendo vya Ubaki na Ngono zembe kutoka na ushawishi wa mavazi hayo
kwa jamii.
Hii kitu ya kutovaa nguo fupi na zile za kuonesha
maziwa nje, inaonekana kuwabana wasanii wa kike moja kwa moja, maana wengi wao
ndio kichocheo kikubwa kwa jamii. Waziri alifunguka na kusema kuwa “hatutaki
uhusike kufanya watu wakutamani au watamani kufanya ngono, hatutaki ushawishi
chochote kwa jinsia ya kiume, kuwa na tabia njema kwa kuvaa kiheshima”.
Pia vyombo vya habari vya Uganda vimekatazwa kuonesha watu
wakipigana mabusu sambamba na wanawake kuvaa hayo mavazi katika vipindi vyao.
Safi sana Yoweri Museveni/ Bado Tanzania sasa. |
1 comment:
Uzembe mtupu kila binadamu anapaswa kuwa na uhuru wa kuvaa kile anachoona kinampendeza na kumridhia kubaka Ni tatizo la akili halihusiani na kivazi cha mtu .mwenye Hili tatizo akitaka kutimiza lengo lake atalitimiza hata kama mwanadada amejiziba mwili mzima. ushauri wa bure tu sio kila kitu ni cha kuigwa
Post a Comment