ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 2, 2014

MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA KUZALIWA KWA CCM MBEYA YAFANA


 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza matembezi ya mshikamano katika kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ,matembezi hayo yalianzia Soweto na kumalizikia kwenye Bustani ya Jiji na baadae zitafuata sherehe katika uwanja wa Sokoine.
  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza kwenye matembezi ya mshikamano katika kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ,matembezi hayo yalianzia Soweto na kumalizikia kwenye Bustani ya Jiji na baadae zitafuata sherehe katika uwanja wa Sokoine.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi wananchi waliojitokeza kwenye matembezi ya mshikamano katika kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti alisema amefarijika sana na matembezi hayo nakuwataka wananchi wa mkoa wa Mbeya waendelee kuwa na mshikamano na umoja kati yao.
 Kila Mtu kwa nafasi yake ameshiriki matembezi ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi.
 Waandishi wa habari maarufu nchi hawakuwa nyuma katika kupata habari za tukio zima la maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM yanayofanyika kitaifa mkoani Mbeya.
 Wanachama na Viongozi mbalimbali wa CCM mkoani Mbeya wakicheza muziki kabla ya kuanza kwa maandamano.
Mwenezi wa CCM mkoa wa Mbeya Ndugu Bashiru Madodi akipuliza Vuvuzela kuashiria mambo yanaenda vizuri wakati wa matembezi ya mshikamano kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM yanayofanyika kitaifa mkoani Mbeya.

3 comments:

Anonymous said...

HAWA WANA KIBALI ?

SPIRIT DIVINERS MINISTRY said...

CHAMA CHA MAPINDUZI NGAO YETU VINGINE VINATUUDHI!!! WE SUPORT IT KWA WINGI WETU

BONIFACE BENNY said...

TUNAKUKUBALI CCM NA RAIS WETU MHESHIMIWA SANA DOKTA JK.... VINGINE VINATUUDHI... TUDUMISHE AMANI, UMOJA NA UPENDO WETU WATANZANIA,,,, VURUGU SIO DILI