ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 19, 2014

MPWA WA MAHITA AJINYONGA UKWENI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile.
Na Dustan Shekidele,Morogoro
MTU mmoja aitwaye Said Mchuma anayedaiwa kuwa ni mpwa wa aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, IGP), Alhaj Omar Idd Mahita ameacha simanzi baada ya kujinyonga ukweni kwa kutumia shuka.
Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita Mtaa wa Tambuka, Kata ya Kingolwira Manispaa ya Morogoro.
Inadaiwa kuwa, marehemu alichukua uamuzi huo baada ya miaka 7 tangu mkewe ambaye hakufahamika kwa jina kufariki dunia.

Baadhi ya watu wa karibu walimwambia mwandishi wetu kuwa tangu alipofariki mkewe, Mchuma hakuwahi kukanyaga ukweni kitu kilichowashangaza wengi walipomuona.

Inadaiwa Mchuma alipofika ukweni alipokewa kisha akaandaliwa sehemu ya kulala, baada ya muda mtu mmoja alimshuhudia akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka na kuwataarifu ndugu na jamaa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Bw. Mohamed Seif alithibitishia kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake.
“Ni kweli tukio limetokea kwenye mtaa wangu na juzi tumemzika kwa kushirikiana na mzee Mahita ambaye ni mpwa wake,” alisema.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Marehemu ameacha mtoto mmoja.

No comments: