MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Crispin Meela, akiongea na Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahmad Msangi huku katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani Mbarak Abdulwazkil akiwasikiliza kwa makini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwazkil, akifungua muziki
Kamishina wa Magereza Nchini, John Minja, katikati pamoja na mkuu wa Magereza mkoa wa Mbeya SACP J.M. Sang'udi wakicheza Twist
MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Crispin Meela, amewataka Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na usalama Mkoa wa Mbeya kutotumiwa na Wafanyabiashara wakubwa katika kuhujumu duka la bidhaa zenye bei nafuu(Duty Free Shop) lililozinduliwa hivi karibuni katika Gereza la Ruanda Mkoani hapa.
Meela alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza na Gazeti hili mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa duka hilo uliofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil,ambapo alisema askari wanaweza kuingia tama ya fedha kwa kuwanunulia bidhaa wafanyabiashara.
Alisema bidhaa zinazouzwa dukani hapo ni mpango wa Serikali kuhakikisha watumishi wake wanakuwa na maisha mazuri kwa kuwafungulia miradi itakayowanufaisha lakini baadhi yao wanaweza kuingia tamaa na kutumika kwa wafanyabiashara wakubwa watakaotaka bidhaa kutoka dukani hapo na kuziuza mitaani.
Alisema kufanya hivyo kutakuwa ni kukiuka sheria na utaratibu wa utumishi wa umma ambapo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani kwa kufungua maduka kama hayo katika Gereza la Ruanda lililofunguliwa jana Mkoani Mbeya, Ukonga-Dar Es Salaam,Isanga- Dodoma,Karanga- Kilimanjaro, Chuo KPF-Morogoro na Butimba- Mwanza.
Kwa upande wake Kamishina wa Magereza Nchini, John Minja, alisema ni ahadi yake kuhakikisha kabla hajaondoka madarakani atahakikisha anafungua maduka kama hayo katika kila Mkoa kwa lengo la kutengeneza maisha ya askari wake.
Alisema baada ya kuzindua duka katika Gereza la Ruanda Mbeya watahamia kanda ya Kusini hususani Mikoa ya Mtwara na Lindi ambako jitihada za kufungua maduka yenye bidhaa za gharama nafuu zitaanza katika kipindi kifupi kijacho.
Na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment