Siku ya jana ndani ya ukumbi wa PTA uliopo ndani ya viwanja vya
maonyesho vya mwalimu JK Nyerere almaarufu kama Sabasaba kulifanyika
maombi maalumu kwa Taifa yakiongozwa na umoja wa makanisa ya
Kipentekoste nchini. Katika maombi hayo yaliyohudhuriwa na waumini
lukuki sambamba na wachungaji wao ilishuhudia askofu Zachary Kakobe
pamoja na Josephat Gwajima wakiongoza maelfu ya waumini waliofika
ukumbini hapo katika kuhubiri neno la Mungu kwa ufupi kisha kuingia
katika maombi ambayo yaliandaliwa vyema na umoja huo.
Credit to Ambwene Mwanjala
No comments:
Post a Comment