Diwani wa Isakamaliwa, Igunga, Doto Kwilasa, Ofisa Mtendaji wa
Kijiji, Erasto Shokoro, wajumbe sita wa serikali ya kijiji na mtu
ambaye hajajulikana wamenusurika kuchomwa moto na wananchi.
Wananchi hao waliwafungia ndani ya chumba cha mikutano viongozi hao
kwa madai ya kuitisha kikao cha kuwazuia vijana wa Isakamaliwa
wasilipize kisasi kwa wafugaji waliowachoma mikuki vijana wenzao.
Vurugu za kutaka kuchoma moto chumba hicho zilitokea juzi katika
Kijiji cha Isakamaliwa baada ya makundi mawili ya wafugaji wa kata hiyo
kutofautiana na kusababisha kundi moja kushambulia jingine kwa mikuki
wakidaiwa kuingiza mifugo kinyume cha sheria katika bonde la Magogo.
Chanzo;Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment