Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili kulia)
akikabidhi funguo ya Pikipiki kwa mmoja wa Makatibu Kata katika Wilaya
ya Kibaha Vijijini,wakati wa shunguli ya kukabidhi Pikipiki 13 kwa
Makatibu Kata na Baiskeli 86 kwa Wenyeviti wa Matawi ya CCM yaliopo
kwenye Wilaya hiyo,Vifaa hivyo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la
Kibaha Vijijini,Mh. Hamoud Abuu Jumaa (kulia).
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili kushoto)
akikabidhi Kadi ya Pikipiki kwa mmoja wa Makatibu Kata waliopo katika
Jimbo la Kibaha Vijijini,wakati
wa shunguli ya kukabidhi Pikipiki 13 kwa Makatibu Kata na Baiskeli 86
kwa Wenyeviti wa Matawi ya CCM yaliopo kwenye Wilaya hiyo,Vifaa hivyo
vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini,Mh. Hamoud Abuu
Jumaa (kushoto).Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani,Ndg. Mwinshehe Shaban Mlawa.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana akikabidhi sehemu
ya Baiskeli 86 kwa Mmoja wa Wenyeviti wa Matawi ya CCM katika Wilaya ya
Kibaha Vijijini.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi,Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa
Jimbo la Kibaha Vijijini,Mh. Hamoud Abuu Jumaa wakiwa wamepanda kwenye
pikipiki hizo kwa kuzijaribu kama ziko vyema kwa matumizi ya Makatibu
Kata waliokabidhiwa.
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha Vijijini,Mh. Hamoud Abuu Jumaa akiwahutubia wananchi
wa Jimbo lake waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya
Msingi Mtongani,kabla ya zoezi la kukabidhi Pikipiki 13 na Baiskeli 86
kwa watendaji wa CCM katika Jimbo hilo.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Pwani,Ndg. Mwinshehe Shaban Mlawa akizungumza machache
kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana
kuzungumza na Wananchi wa Kibaha Vijijini.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa
kuwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Kibaha Vijijini,Mkoani Pwani,ambapo
amewataka Wananchi hao kutowaonea haya Watendaji wao iwapo watafanaya
mambo ndivyo sivyo.
No comments:
Post a Comment