Na Boniface Wambura, TFF
Mechi
ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri
iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imeingiza
sh. 448,414,000.
Mapato
hayo yametokana na watazamaji 50,202 waliokata tiketi kushuhudia
pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh. 25,000 na sh.
35,000. Yanga ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.
Mgawo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) ni sh. 68,402,135.59, gharama za kuchapa tiketi ni sh. 10,343,219,
waamuzi na kamishna sh. 14,665,930 na matangazo sh. 15,679,000.
Uwanja
sh. 50,898,557.31, gharama za mchezo sh. 33,932,371.54, Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)/Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 33,932,371.54 wakati Yanga ilipata mgawo wa sh. 220,560,415.01.
Nayo
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting
iliyochezwa jana (Machi 2 mwaka huu) imeingiza sh. 20,610,000 ambapo
kila klabu ilipata mgawo wa sh. 4,402,492 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,143,898.31.
MECHI YA MLALE, LIPULI YARUDISHWA NYUMA
Mechi
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Mlale JKT na Lipuli iliyokuwa
ichezwe Machi 9 mwaka huu Uwanja wa Majimaji mjini Songea sasa itachezwa
Machi 5 mwaka huu.
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko hayo ili kuipunguzia
gharama timu ya Lipuli ya Iringa ambayo jana (Machi 2 mwaka huu)
ilicheza mechi mjini Songea dhidi ya Majimaji
No comments:
Post a Comment