Miss
Tanzania 1999, Hoyce Nambuo Temu akiwasili katika Viwanja vya Mahakama
ya Wilaya ya Temeke akiongozana na Mama wa marehemu Emmanuel, Hilda Lewi
Nambuo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) Dkt. Helen Kijo Bisimba akiongea jambo na Hoyce Temu.
Wanaharakati mbalimbali wakijadiliana jambo nje ya mahakama wakati wa mapumziko ya kusikiliza kesi hiyo.
HUKUMU ya kesi ya familia ya Miss Tanzania 1999, Hoyce Nambuo Temu,
kuhusu mzozo mkubwa wa wapi pa kumzikia mwanafamilia mwenzao, Emmanuel
Lewi Nambuo Temu (33) aliyefariki dunia Februari 16 mwaka huu katika
Hospitali ya Temeke, Dar imetolewa leo katika Mahakama ya Wilaya ya
Temeke ambapo Mama wa marehemu Emmanuel, Hilda Lewi ameshinda!
Mama wa marehemu Emmanuel, Hilda Lewi Nambuo alikuwa anashikilia
msimamo kwamba, mwanaye akazikwe kwenye makaburi waliyozikwa mababu zao
yaliyopo kwenye eneo la Kitahire, Old Moshi, Kilimanjaro lakini mjomba
mtu aitwaye Jacob Nambuo Temu alikuwa akipinga.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kassim Mkwawa na
mwili wa marehemu uliokuwa bado umehifadhiwa Hospitali ya Temeke
utazikwa eneo la Kitahire, Old Moshi mkoani Kilimanjaro.
(PICHA / HABARI: HARUNI SANCHAWA / GPL)
No comments:
Post a Comment