Baraza la Vyama vya Siasa Nchini limedai kuwa mvutano unaoendelea ndani ya Bunge Maalum la Katiba unachangiwa kwa kiasi kikubwa na makundi yasiyo rasmi ya wanasiasa ambayo kwa bahati mbaya yanatambuliwa na Uongozi wa Bunge hilo. Madai hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Kuga Mziray katika mkutano na wanahabari uliofanyika mjini Dodoma leo.
No comments:
Post a Comment