Mama Salma mgeni rasmi hafla ya wanawake mashuhuri nchini
Imeandaliwa na Vodacom kupitia “Connected Women”.
Lengo kuwasaidia wanawake wasio na mafanikio
Dar es Salaam, Machi 4, 2014 …Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete kesho(Jumatano Machi 5, 2014) anaongoza
hafla inayowakutanisha wanawake zaidi ya 250 kutoka kada mbalimbali
wakiwemo wasomi, wake wa viongozi, wajasiriamali, wanasiasa kuangalia
mafanikio ya ukombozi wa kiuchumi na kijamii wa mwanamke hapa nchini.
Wanawake
hao wanakutana chini ya kile kinachoitwa “Connected Women” ya Kampuni ya
Vodafone ambapo kupitia hafla hiyo wanawake hao watajadali mchango wa
teknolojia ya simu za mkononi na jinsi ilivyobadili maisha ya wanawake
hapa Tanzania kupitia miradi inayofadhiliwa na Vodacom Foundation.
“Shabaha ni
kujenga daraja kwa wanawake wenye mafanikio kwa umoja wao kujenga hamasa
na kuwawezesha wenzao wasio na mafanikio kufikia mafanikio ili kuondoa
pengo la utofauti wa jinsia lililopo ndani ya jamii hususani sekta ya
elimu, afya, uchumi na uongozi.”Alisema Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na
Uhusiano wa Vodacom Tanzania Georgia Mutagahywa. .
Usawa wa
kijinsia imekuwa ni ajenda ya muda mrefu katika mataifa mbali mbali
duniani ambapo mengi yao wanawake wamekuwa wakinyimwa fursa za msingi
ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kuleta mafanikio ya kasi kwa
jamii husika
Mama Salma
Kikwete anatarajiwa kuwakutanisha wanawake hawa ambao wamefanikiwa kwa
kuwezeshwa kupata fursa za kielimu, kiafya, kiuchumi na uongozi mpaka
kuwa watu muhimu na wanaotambulika ndani ya jamii ya watanzania
Hafla hiyo
inayofadhiliwa na Vodacom ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake
dunaini inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.
Mutagahywa
aliongeza kuwa “Wapo wanawake wenye nyadhifa kubwa serikalini, katika
sekta binafsi pamoja na mafanikio ya kiuchumi ambapo kwa umoja wao
wakiamua kutumia nafasi walizonazo wanaweza kumkomboa mwanamke mwenzao
kutoka katika tanuri la usawa wa kijinsia.”
Utofuati
huu wa kijinsia pamoja na sababu nyengine unachangiwa pia na mila potofu
zilizopitwa na wakati ambazo siku zote zinamkandamiza mwanamke na
kumfanya abaki nyuma katika shughuli zote za kimaendeleo huku zikimpa
nafasi zaidi mwaname”. Alisema.
Miongoni mwa
mafanikio ambayo teknolojia ya simu za mkononi katika kubadili maisha
mpango wa M-pesa wa kuwawezesha wanawake mikopo nafuu isiyo na riba –
MWEI, mradi wa fistula katika hospitali ya CCBRT,
No comments:
Post a Comment