ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 7, 2014

SAMAHANI KWA PICHA ZA KUTISHA...MCHAWI APIGWA HADI KUFA MBEZI NI BAADA YA KUDONDOKA NA UNGO


WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia.




Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina.
Kabla ya kufariki alisema “mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu”.
“Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu”. 
 
Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao.

 Kwa mujibu wa mashuhuda wengine wa tukio hilo walisema baada ya kuanguka eneohilo walimkimbiza hadi ndani kwa mtu na kumtoa pamoja na zana zake za kichawi ambapo walizichoma kwanza moto ikiwa pamoja na ungo wenyewe ndipo wakaendelea kumpiga kwa mawe hadi mauti yalipomkuta.

 “Huyu jamaa bwana, ameanguka hapa, sasa kwakuwa sisi hatuna mzaha na watu kamahawa tumemtoa huko alikokimbilia na kumhalalisha kwa vijana wa kazi hapa baada ya kuhakikisha zana zake zote tumezichoma moto” alisema mkazi mmoja wa maeneo hayo. Hata hivyo baadhi ya wananchi walielekeza lawama zao kwa Jeshi la Polisi (Kituo cha Polisi Kimara) kilichopo Mbezi kwa Yusuph kwa kuchelewa kuja kumuokoa kija huyo ingawa walipewa taarifa mapema. 
“Sisi tumepiga simu kituoni hapo hata kabla huyu mchawi hajaanza kushambuliwa, lakini angalia tukio limeanza saa 12 asubuhi wanakuja baada ya masaa mawili, huu nu uzembe” alisema mkazi wa eneo hiloaliyejitambulisha kwa jina moja la Ali.

Ingawa katika tukioa hilo kulitokea mkazi mmoja aliyekuwa na silaha aina ya bastola na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatawanyisha wananchi hao wenye hasira kali, haikusaidia kitu kwani waliendelea kumpiga hadi wakahakikisha amekufa.

Mtanzania lilibisha hodi katika kituo cha Polisi Kimara ambacho mwili wake ulipelekwa ili kupata uthibitisho zaidi lakini askari wa zamu waliokuwa mapokezi walisema hawana mamlaka ya kutoa maelezo hadi mkuu wa kituoa au mkuu wa makosa ya kieupelezi wa kituo hicho ndiyo wenye dhamana.

 Aidha wakuu hao OC CID (ASP) M. Mganga pamoja na Mkuu wa kituo wote hawakuwapo kituoni wakati Kamanda wa kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga hakuweza kupatikana ili kudhibitisha tukio hilokutokana na namba yake ya simu kuita bila kupokel

1 comment:

Anonymous said...

Hivi na huyo mlalamikaji analalamikia nini jeshi la polisi kuhusu huyo mchawi kuuawa? Kwani na wa wanapoua watu kichawi je? Zamu yake imefika kama hasingekufa hiyo siku angeua mtu/watu wengine wasio na hatia pia. Kuua ni kuua tu tofauti ni kwamba huyu amapigwa mpaka kufa na mchawi anaua kwa kutumia mauchawi yao wajuavyo wenyewe lakini jibu ni kwamba mtu nakufa; ndo maana tunaona kama ni makosa kumuua kwa vile hatuwaoni wanapoua watu. Lakini hawa wachawi wanaua watu kila siku kupitia ajali, nk. Au huyo anayetetea ni mchawi mwenzie? Waswahili usema, chongo kwa mnyamwezi, kwa mswahili ni amri ya Mungu.