Msemaji wa Hazina Capital, Rachel Ndauka (kulia) na William Joseph (kushoto) wakiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Hazina Capital tunapenda kujitambulisha/kuwatangazia Watanzania juu ya soko jipya la biashara litakalojumuisha wafanyabiashara wa bidhaa za aina mbalimbali kutoka Kariakoo na kuwapa nafasi ya kuonyesha pamoja na kuuza bidhaa zao Coco Beach ambalo tumeliita ‘Kariakoo at Coco Beach’ linalotarajiwa kuanza kuanza Machi 29 na 30 mwaka huu na kila mwisho wa wiki ya mwisho wa mwezi.Soko hili litatatoa nafasi pia kwa wananchi ambao huwa hawaendi Kariakoo au hata wanaoenda, kununua bidhaa zinazopatikana Kariakoo katika ufukwe huo wa bahari na kwa bei ileile na hata ya chini zaidi.
Pia watu wanaweza kuja na familia zao kwa sababu kutakuwa na vitu vingi kama michezo ya watoto na n.k.
Lengo la soko hili siyo kuwafanya watu wanunue tu, bali pia kuwasogezea karibu zaidi wananchi huduma ili waweze kupata mahitaji yao katika mazingira mazuri ya utulivu, ya furaha na usalama.
Pia lengo letu ni kuendeleza na kukuza wafanyabiashara pamoja na kupanua zaidi masoko yao lakini pia kuwawezesha kufikia malengo na mafanikio na kulitangaza soko letu maarufu la Kariakoo, Tanzania.
Hazina Capital inapenda kuwashukuru waandaaji wenza ambao ni Ndauka Promotion na Real Stars pamoja na Hazina Lounge kuturuhusu kutumia mahali hapa.
Tunapenda kuvishukuru vyombo vya habari kwa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment