ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 6, 2014

WATOTO WAMUUA KINYAMA MPENZI WA MAMA YAO MKOANI KATAVI


Ndugu wawili wa kiume wa familia moja wilayani Mlele mkoa  wa Katavi, wanatuhumiwa kumuua mpenzi wa mama yao kwa kumchinja, kisha kutelekeza mwili wake porini. 
Wakazi hao ambao mmoja ni mtoto mwenye umri wa miaka 16 ni wakazi wa Kitongoji cha Milumba  Kata ya Kibaoni na aliyeuawa ni Kitungulu Luhende (65). 
Inadaiwa  mama yao, Sai Mponje (65) ambaye  ni mjane anayeshikiliwa na polisi kwa sasa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Luhende, jambo ambalo watoto hao hawakufurahishwa. 
 Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari  alitaja  watuhumiwa hao ni Nyengu Kashele (19) na nduguye mwenye umri wa miaka 16.  Mtoto huyo anashikiliwa wakati Nyengu amejificha kusikojulikana. 
Mwili wa marehemu uligundulika Machi 3, mwaka huu saa 3:30  asubuhi  katika  milima ya  kitongoji  hicho  cha Milumba  ukiwa umeharibika.
Mwili huo  uligundulika  kutokana na msako uliofanywa  na askari wa jadi (sungusungu) kwa kushirikiana na polisi na wananchi.
Kidavashari  alisema  Februari  22,  mwaka  huu  saa  2  asubuhi, Luhende ambaye pia  ni mkazi  wa kitongoji  hicho  cha Milumba,  alimuaga  mkewe  kwamba anakwenda kijiji cha  Kirida  ambako ana mke mwingine. 
Hata hivyo, Kamanda alidai kuwa  badala  ya kwenda  kijijini Kirida,  aliko mke wake mwingine,  kwanza  alipitia nyumbani  kwa rafiki  yake  katika  kitongoji  hicho  cha Milumba, aitwae Milembe Katembeni  ambako  aliacha pikipiki  yake  yenye  nambari za usajili T449 BAF. 
Inadaiwa kisha alikwenda moja kwa moja kwa Sai (mama wa watuhumiwa). Kamanda alisema tangu hapo hakuonekana hadharani hadi mwili ulipokutwa umetelekezwa eneo  la  milimani huku pembeni kukiwa na leseni yake ya udereva. 
Akielezea sababu za kuanza kumtafuta, Kamanda alisema baada ya  kutorejea  kwa rafiki yake kuchukua pikipiki, Katembeni  aliingiwa  wasiwasi  ndipo Machi 2 , mwaka huu  aliamua kutoa  taarifa kwa kiongozi wa sungusungu na  kisha polisi, na msako ukaanza.CHANZO ZIRO BLOG

No comments: