\
Jeneza likiwa na mwili wa Marehemu tayari kwa Ibada ya Mazishi iliyofanyikia Nyumbani kwao Chiwanda. |
Mchungaji wa Kanisa la Africa Mission Church wanakosali wazazi wa Marehemu akiongoza ibada ya Mazishi. |
baadhi ya Waombolezaji wakielekea Makaburini. |
Joseph Mwaisango akiwa amebeba Jeneza lenye mwili ya marehemu kuelekea Makaburini tayari kwa safari ya mwisho |
Mwili wa Marehemu ukishushwa kaburini. |
Kaburi likifukiwa baada kukamilika kwa taratibu zote ambapo mwili wa marehemu ulizikwa katika makaburi ya Kijiji wanakozikwa Wananchi wengine. |
Kwa mujibu wa mila za kabila la Wanyamwanga vijana hawa walikuwa wakisiliba kaburi baada ya kumaliza mazishi. |
KATIKA
hali ya kusikitisha Watoto wawili kati ya Wanne ambao ni mapacha
waliozaliwa kwa pamoja na mwanamke Aida Nakawala Mkazi wa Kijiji cha
Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya wamefariki dunia kwa ugonjwa wa
Nimonia.
Watoto
hao wamefariki kwa mida tofauti ambapo Mtoto wa Kwanza alifariki
Nyumbani kwao baada ya kuugua ghafla ndipo hali za wengine zilipoanza
kutia shaka na kulazimu Waandishi wa Habari wa Mtandao wa Mbeya Yetu, Gazeti la Jambo Leo na Redio ya Bomba Fm waliohudhuria mazishi ya Mtoto huyo kulazimika kuwakimbiza katika Hospitali ya Wazazi Meta kwa matibabu zaidi.
Hata
hivyo baada ya kupokelewa kwa watoto hao Watatu mtoto mmoja aliaga
dunia baada ya kuchelewa kupata matibabu kutokana na kubanwa na kifua na
kusababisha kushindwa kupumua vizuri.
Hali
za watoto wawili waliobaki wanaendelea vizuri na matibabu na kwa mujibu
wa Daktari anayewatibu amesema taratibu za Hospitali hiyo ni kupokea
watoto waliochini ya Miezi miwili lakini hao wamezidi umri huo hivyo
badala ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya wataendelea kuwepo Meta
hadi hapo hali zao zitakapoimarika.
Baadhi
ya wananchi na wauguzi katika Hospitali ya Wazazi Meta wamesema sababu
ya watoto hao kuugua ni kutokana na kukosekana kwa uangalifu wa karibu
katika malezi ya watoto hao ukilinganisha na maisha ya vijijini kukosa
watu wenye uelewa wa afya za watoto.
Wengine
wameitupia lawama moja kwa moja Serikali kwa kushindwa kuchukua hatua
za haraka tangu watoto walipozaliwa ili kujiridhisha na mazingira
wanayopaswa watoto hao kuishi kwa kuwapatia msaada wa karibu na ushauri
wa kitaalamu.
Kwa
upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya, Thobias Mwalwego,
alikiri kuwepo kwa urasimu katika Idara yao kwa madai kuwa tangu watoto
hao walipokuwa wamezaliwa walipata taarifa na kuchukua hatua kwa afisa
mmoja kufika kijijini na kuchukua picha zao.
Alisema
urasimu unakuja kutokana na Ofisi ya Wilaya na Mkoa kukosa fungu la
dharula ambapo barua za maombi zote hupelekwa makao makuu kwa Kamishna
wa Ustawi wa Jamii ambapo Ofisi yake huchukua muda mrefu kurudisha
majibu kutokana na waombaji kuwa wengi.
Alisema
kila ofisi katika Ngazi ya Mkoa ingekuwa na fungu la Dharula kama
ilivyo katika Ofisi zingine hali ambayo ingeweza kusaidia kuepusha vifo
vya watoto hao kutokana na kupatiwa msaada wa ushauri na makazi rafiki
kwa malezi ya mapacha wanaozidi wawili.
Aidha
alishauri kila Halmashauri Nchini kutenga bajeti za kusaidia majanga
kama hayo na vitu vya dharula wakati Serikali inajipanga kutekeleza
kutokana na taratibu zake kuchukua muda mrefu ili kuweza kukabiliana na
hali yoyote na muda muafaka.
Meneja
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Ahmed
Issa katikati na Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu Blog wakimkabidhi Aida
Nakawala msaada wa pesa kiasi cha shilingi laki tano 500,000/ toka wa
watanzania waishio nchini Uswisi
|
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Kanda ya Nyanda za Juu kusini wakiwa wamewabeba watoto hao
|
Joseph
Mwaisango alipokwenda kuwatembelea Hospitali ya wazazi Meta watoto
wawili waliobakia na hali zao kwa sasa zinaendelea vizuri
|
Akikabidhi
msaada huyo kwa mama huyo kijijini kwao Chiwanda Wilayani Momba, Meneja
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Ahmed
Issa kwa niaba ya Watanzania hao alisema wameguswa sana na hali hiyo na
kuahidi kuendelea kuchangia kila mara.
Aidha alisifu utendaji kazi wa Waandishi wa Habari hususani Mbeya yetu Blogwaliofanikisha
kuibua jambo hilo na kulitolea taarifa kila wakati jambo lililosaidia
kufahamisha watu wengi wakiwemo wanaoishi nje ya Tanzania na kutuma kile
wanachokuwa wameguswa nacho.
Mbali
na Hilo, Meneja wa TMA Kanda ya Mbeya, Ahmed Issa, pia amejitolea
kuusafirisha mwili wa Marehemu kutoka Hospitali ya Meta Mbeya hadi
Kijijini kwao Chiwanda Wilayani Momba kwa ajili ya taratibu za Mazishi.
Picha na habari na Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment