DUNIA
ina mengi, hili nalo moja wapo! Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na
miaka 35 amekutwa porini akiwa uchi wa mnyama na hawezi kuongea hali
iliyozua hofu kwa wananchi na kudai ni msukule.
Tukio
hilo lilijiri hivi karibuni maeneo ya Pugu Mnadani, wilayani Ilala
jirani kabisa na Pori la Hifadhi ya Kisarawe mkoani Pwani. Baadhi ya
wakazi walimhusisha mwanamke huyo na imani ya msukule wakidai huenda
alitoroka kutoka kwenye makazi yake kabla ya kukatwa ulimi.
Akizungumza
na paparazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo, Said alisema baada ya kumkuta
katika hali hiyo walianza kwa kumsitiri kwa nguo kisha mwanamke mmoja
mganga alimlisha dawa ya kienyeji ndipo akaanza kuzungumza lakini kwa
shida.
“Tulimuuliza
jina lake akasema anaitwa Tumsifu Yesu. Alidai ameishi kwenye pori hilo
kwa kipindi kirefu bila kujua alifikaje kwa vile kwao ni Iringa. “Cha
kustaajabisha zaidi pale alipopewa chakula alifanikiwa kula maandazi
arobaini na maji lita tano ndani ya dakika kumi tu,” alisema shuhuda
huyo.
Akaendelea:
“Baada ya kumaliza kula alionesha ishara ya msalaba kwa kumshukuru
Mungu. Ndipo akapelekwa serikali ya mtaa na baadaye Kituo cha Polisi cha
Pugu kwa msaada zaidi,” kilisema chanzo hicho
No comments:
Post a Comment