ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 11, 2014

KABURI LA SHEIKH YAHYA HUSSEIN LAFUKULIWA


Kaburi la Shekhe Yahya Hussein amezikwa tarehe 21.5.2011.

Kaburi la Sheikh Yahya Hussein ambaye alizikwa tarehe 
21.5.2011.

 Makaburi mawili ya Sheikh Yahya Hussein na Sheikh Kaseem Bin Jumaa yamevunjwa na mgambo wa jiji saa nane usiku eneo la Tambaza, makaburi ambayo yana muda mrefu katika eno hilo.



 Hata hivyo haijajulikana chanzo cha kuvunjwa kwa makaburi hayo.

 Wakiongea na waandishi wa habari baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya vyakula eneo hilo wamedai kuwa, walifika asubuhi na kukuta hali hiyo ya kuvunjwa kwa vibaraza vya maduka yao pamoja na kuvunjwa kwa makaburi hayo mawili ya watu masheikh mashuhuri hapa nchini.
Kaburi la Shekhe Kasimu Bin Juma amezikwa mwaka 1994
Kaburi la Sheikh Kaseem Bin Juma ambaye alizikwa 
mwaka 1994.

 Naye mtoto wa marehemu Sheikh Yahya Hussein, Bi. Mariam Hussein alifika katika makaburi hayo na kujionea kwa macho yake jinsi kaburi la Baba yake lilivyobomolewa.

 Mariam amesema anasikitishwa sana kwa kuvunjwa kwa kaburi la Baba yake bila ya sababu ya msingi.

Mtoto wa Marehu Shekhe Yahya Mariam Yahya Husein akitafakari jambo kwenye eneo alilozikwa Baba yake Mzazi.
Mtoto wa Marehem Sheikh Yahya Hussein,  Mariam Yahya 
Hussein akitafakari jambo kwenye eneo 
alilozikwa Baba yake mzazi

1 comment:

Anonymous said...

Haiingii akilini kweli kiongozi gani anaweza kutoa amri ya kuharibu makaburi!!! Hivi utu uko wapi, tunashindwa hata kuheshimu marehemu. Watu tunasahau kwamba iko siku nasi makaburi yatakuwa ndiyo makazi yetu!!??

Kero za kweli za wananchi zinafumbiwa macho, wanaonewa marehemu ambao hawana uwezo wa kujitetea!! Inashangaza matatizo kama ya Garage bubu katika makazi ya watu zimeshindwa kushughulikiwa kwa zaidi ya miaka ishirini sasa. Hao mgambo wanashindwa kuwaondoa wenye garage bubu? Hizo ndizo kero ambazo tunataka serikali izishughulikie, siyo kuvamia marehemu wa watu na kuvunja makaburi yao.