Katika kipindi cha ALA za ROHO cha CLOUDS FM, Mtangazaji/Msanii Diva The Boss akiwa na Rapper WAKAZI alisema kuwa, NIKKI MBISHI ni msanii mzuri sana na anafanya vizuri ila yeye binafsi anachoona ni kwanini anakosa kuwa na heshima kwa wasanii wenzake na watu wengine sio jambo zuri na aanze kuwa na RESPECT, na hii ni kutokana na matendo anayodai ya sio kuwa na heshima ya kuandika na kudiss wasanii wenzake kwenye mitandao ya kijamii. WAKAZI nae alisema yeye hana beef na msanii yoyote na anashangaa madai ye yeye kuwa na ‘Beef’ na msanii Nikki Mbishi na Godzillah. Vile vile alisema kuwa wasanii wengi wanaotaja majina ya watu kwenye nyimbo zao mara nyingi hutakaga attention kwa kutumia majina ya watu kwenye nyimbo zao ili wasikike, wakazi hakutaka kuiongelea sana hiyo issue na wasanii hao wakatoka kwenye hiyo topic.
WAKAZI msanii ambae ameanza muziki wake muda mrefu kidogo akiwa kule nchini Marekani na ametoka kuachia nyimbo zake mbili kwa mpigo, “Sexy Lady” na “Sumu ya Panya”, alisema Tanzania hatuna uzalendo wa kusifia na kusupport cha kwao. hii ni kutokana na swali aliloulizwa na Diva kuwa, kwanini nini tunasupport sana nyimbo za Nigeria na zinapigwa sana kwenye Clubs za hapa nchini kuliko nyimbo za wasanii wa hapa nyumbani.
Wasanii hawa walizungumzia jinsi gani nchi kama Uganda inavyosupport wasanii wao kwa kazi zao na hata show zao na kuwafanya wasanii hao kuweza kuwa na maisha mazuri na kuweza kuendelea kutengeneza muziki mzuri wenye hadhi ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment