Mwenyekiti wa Taifa
wa Chama cha Wasioona (TLB) Mwalimu Greyson Mlanga(aliyesimama) akitoa
somo juu ya Warsha ya Siku mbili ya Mkatabawa Umoja wa Mataifa Kwa Watu
Wenye Ulemavu Mjini Ifakara hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Chama Hicho Wilaya ya Kilombero Maria Faya na Kulia ni Mwalimu Janet
Kalalu, Mratibu wa Chama Wilaya.
Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero
Watu wenye Ulemavu nchini Tanzania wametakiwa kushiriki katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa muuujibu wa Uwezo wao.
Akizungumza katika
Warsha ya Siku mbili iliyofanyika Mjini Ifakara Wilayani Kilombero hivi
karibuni Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona (TLB) Taifa Mwalimu Greyson
Mlanga amesema kuwa ni vyema watu wenye Ulemavu wakashiriki katika
shughuli hizo ili kusaidia Jamiii kuondokana na Dhana ya kuwa Walemavu
ni watu omba omba.
Mwenyekiti huyo
amesema kuwa ushirikiano wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu ndiyo njia
pekee ya kujikwamua katika maisha huku akisisitiza upatikananji wa
Takwimu sahihi za Watu wenye Ulemavu ili ziweze kusaidia maendeleo ya
Watu wenye Ulemavu.
Katika Mafunzo hayo
yaliyoshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Madiwani, Watendaji na
Wawakilishi wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Mwenyekiti huyo alielezea
umuhimu wa kupata Elimu na kujua Haki za Watu wenye Ulemavu.
Mafunzo hayo
yaliyoandaliwa na Chama cha Wasioona (TLB) Wilaya ya Kilombero
yameshirikisha Wadau kutoka Kata za Ifakara, Kibaoni, Kiberege na
Kisawasawa yalifadhiliwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society.
Viongozi wa TLB
Taifa Wakiungana na Viongozi wa TLB Wilaya ya Kilombero katika kuimba
Wimbo wa Haki za Binadamu katika Mafunzo ya Siku Mbili yaliyowakutanisha
Wadau mbalimbali, Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Wilaya ya Kilombero,
uliofanyika hivi karibuni Mjini Ifakara. Kutoka Kushoto ni Maria Faya,
Mwenyekiti wa TLB Wilaya ya Kilombero Maria Faya, Mwalimu Robert
Bundala,Makamu Mwenyekiti Wasioona Taifa, Mwenyekiti wasiona Taifa
Mwalimu Greyson Mlanga na Mratibu wa Wasioona Wilaya ya Kilombero
Mwalimu Janet Kalalu.
Washiriki wa Mafunzo
ya Siku Mbili ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa Juu ya Watu Wenye Ulemavu
wakiwa kwenye Picha ya pamoja na Viongozi wa Taifa wa Chama cha Wasiona
(TLB) Mjini Ifakara Hivi karibuni.(PICHA ZOTE KWA HISANI YA HENRY
BERNARD MWAKIFUNA WA IFAKARA).
No comments:
Post a Comment