Meneja wa kituo cha
Kahama FM Redio, Marco Mipawa, akiwakaribisha washiriki na kufungua
warsha ya mafunzo ya siku nne ya waandishi wa habari na watangazaji wa
Redio Jamii kuhusu kuandika taarifa za Maafa na Misaada ya Kibinadamu
yanayofanyika mjini Kahama. Kushoto ni Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu na kulia ni Hellen Msemo kutoka Mamamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA).
Na Mwandishi Wetu
Ukosefu wa taarifa na
lugha sahihi halikadhalika kukosa uelewa katika jamii ni miongoni mwa
mambo yanayosababisha kutokea kwa maafa.
Katika mada inayohusu
Misaada ya Kibinadamu na Taarifa za Maafa katika mafunzo ya siku nne ya
wanahabari na watangazaji wa redio jamii mjini Kahama Mratibu wa idara
ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Harrison Christopher
Chinyuka alisema jamii lazima ifahamu historia ya maeneo yanapotokea
maafa na wapate elimu ya kutosha ili waweze kuepusha maafa asili.
Bwana Chinyuka alisema
kwamba hilo litafanikiwa iwapo waandishi wa habari watawajibika
kikamilifu kwa kuandika taarifa za majanga na maafa ambazo ni sahihi na
kwa wakati kwa sababu wakati mwingine wamekuwa wakishindwa kutumia lugha
sahihi ya kusheheneza taarifa husika.
Mratibu wa Idara ya
Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Harrison Christopher Chinyuka
Chinyuka, akiendesha mafunzo kwa waandishi na watangazaji wa Redio za
Jamii nchini.
“Wanahabari wana
mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa madhara ya maafa yanapunguzwa kwa
kuipa uelewa jamii husika kwa kutoa taarifa na lugha sahihi zinazohusu
maafa ili kutoa nafasi kwa wahanga kujihami ipasavyo”, alisema Bwana
Chinyuka.
Wajibu wa mwandishi wa
habari katika kupunguza maafa ni kukuza uelewa wa jamii kuhusu hatua za
hatari, kuzuia na kukabiliana na maafa, kukubaliana juu ya viwango vya
taratibu za uendeshaji katika sehemu ya maafa.
Wajibu mwingine ni
kusambaza ujumbe wa onyo kwa kuaminika na haraka iwezekanavyo na
kuiweka jamii vizuri kitaarifa wakati huo huo kuepuka uvumi na hofu
katika hali ya hadhari.
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu, akihamaisha washiriki katika vikundi kazi.
“Wajibu wenu waandishi
wa habari kabla, wakati na baada ya maafa ni kutimiza jukumu la kulinda
na kusaidia kuunganisha familia na kujenga kujiamini, sio kuachia
mchakato njiani”, alisema Bwana Chinyuka.
Madhumuni ya mafunzo
hayo ni kutoa uwezo kwa waandishi wa habari na watangazaji wa redio
jamii kuandika taarifa zinazohusu kutoa msaada wa kibinadamu na
kupunguza madhara yatokanayo na majanga na maafa nchini katika mradi
unofadhiliwa na shirika la maendeleo ya Sweden (SIDA) kwa kushirikiana
na UNESCO.
Mafunzo hayo
yanatekeleza malengo ya UNESCO linalohusisha kuimarisha uwezo wa kukuza
mazingira ya uhuru wa kujieleza kwa ajili ya maendeleo, kuendeleza
demokrasia na utamaduni wa mazungumzo ya amani bila migogoro.
Hellen Msemo kutoka Mamamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Mwandishi na
mtangazaji kutoka kituo cha Redio O.R.S FM ya Simanjiro, Julius Laizer,
akichangia maoni wakati wa mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO.
Picha juu na chini ni
sehemu ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo kwa umakini
yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa
kushirikiana na UNESCO.
Mafunzo yakiendelea.
No comments:
Post a Comment