Nchini Kenya kuna Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Naivasha ambae katengeneza ‘Ndege’ yake ambayo toka ameanza kuiunda alisema lazima ipae huku akiwa katumia vifaa mbalimbali kutoka kwenye Bajaji kuiunda.
Mzigo ulipokamilika nyumbani kwao alipoitengenezea, Polisi wa mji huo
wakamkataza kuipaisha kwa sababu ni kinyume na sheria lakini ili
kuepuka kumkatisha tamaa… wakamwambia ni vyema akapata kibali kutoka kwa
mamlaka ya anga.
Paul Karanja alizuiwa na polisi kuipaisha hii ndege kutoka uwanja mdogo wa ndege wa Karagita na kuwanyima uhondo zaidi ya watu 500 waliofika asubuhi ya saa 3 kuangalia chombo kikipaishwa.
Hata hivyo Mwanachuo huyu wa chuo kikuu cha Meru ana imani ataipaisha ndege yake siku moja ili kutimiza ndoto yake ambayo hata hivyo ilipata hitilafu kwenye uwanja wa ndege wa Karagita kutokana na hali mbaya ya uwanja huo iliyosababisha tairi la ndege yake kuharibika.
Karanja ambae ni Mwalimu pia wa shule ya upili, amesema tayari ameiandikia barua mamlaka ya ndege nchini Kenya kuhusu kupaisha ndege hiyo lakini hajapata majibu
3 comments:
Huyu bwana anatengeneza ndege ya karne gani, ashukuru hao polisi la angetuletea another Malaysian Airline.
Du, nilidhali ndege inapaswa kuwa na instruments, etc hii ya mshikaji kali.kiti chenyewe kachukua kwenye bar ya Masawe sijui km kita resist upepo mkali huko juu..tunamtakia mafanikio mema.
watu wengine kwa majungu ! anagalau mwnzenu kajaribu something kuliko nyinyi mnatengeneza majungu tu, mtakienikila la kheri mwenzenu jamani, Khaaa! roho gani hizo!!
Post a Comment