Wasanii wengi wa fani mbali mbali kuanzia filamu hadi bongo
fleva, wamekuwa wakipoteza mashabiki wao wengi kutokana na ile hali tu
ya jinsi anavyochukulia umaarufu wake, kama anatumia umaarufu wake
vizuri basi hutokea kupendwa sana na watu hata wale ambao siyo mashabiki
wake, watampenda tu kama mtu wakawaida.Kismati hiki cha kupendwa sana
na watu wa rika mbalimbali anacho naye msanii mkongwe sana Ali Kiba.
Ukimuongelea Msanii kama Ali Kiba, watu wengi wanatamani wasanii wote
wawe kama yeye,ni mmoja kati ya wasanii wachache sana maarufu ambao
hawana ulimbukeni wa mali au umaarufu wao, cause wengi wao pale wapatapo
umaarufu kidogo tu, huanza kudharau watu wake wa karibu, haswa wakipata
mali kidogo basi huishia kuonyesha watu magari na
nyumba,hata kama
haiwahusu, ilimradi tu basi nao waonekane kama wasanii wa nje wenye mali
zao, ila kwa Ali kiba imekuwa ni tofauti sana,na hiki ndicho
kinachofanya AliKiba aweze kupendwa zaidi na kila mtu.
Kupitia mtandao wa instagram Ali kiba aliweza kuweka wazi mtazamo wake wa mafanikio:
“Kuishi maisha halisi yenye furaha na maana kwako ni kitu cha thamani
sana. Unayo kila sababu ya kufuata njia yako ya maisha yenye misingi
mizuri ya kukujenga katika kila nyanja ya maisha yako. Kwa kuwa kila mtu
ana maono yake binafsi kuhusu maisha ni vigumu kufafanua maana halisi
ya maisha. Naamini nawe pia una falsafa yako ya kutafsiri nini maana ya
maisha mazuri kwako,”
“ 1. Kuwa mkweli kwako mwenyewe. -Maisha mazuri hutafsirika na mtu
mwenyewe, labda mimi naweza kukuambia maisha mazuri kwangu ni kuwa
mwenye furaha na familia yangu, mpenz wng afya njema, kijana mtanashati,
hodari na mwenye kujitegemea mwenyewe. Nawe pia una maono yako labda ni
tofauti na yangu, ni hayo maono yako ndiyo yanayokutambulisha na
kukufanya uishi kwa misingi uliyojiwekea. “
“Faraja katika maisha yako hupatikana pale unapopata ulichokuwa
ukikitamani kwa muda mrefu. Lakini pia faraja hii huletwa na kuongezeka
zaidi pale wewe mwenyewe kutoka moyoni mwako unapoamua kufurahi kwa kile
kidogo au kikubwa ulichonacho.”alimalizi Ali Kiba. Na kwa mtazamo huu
utaona ni jinsi gani kuna utofauti wa wasanii wengine wengi na msanii
huyu wa kipekee mkongwe sana kwenye game la Bongo music.
No comments:
Post a Comment