ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 11, 2014

Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii

Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii (CISNA) wakiendelea na Mkutano huo uliofunguliwa rasmi jana April 10, 2014 na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Peter Ilomo (katikati mwenye tai nyekundu).

Na Mwandishi wetu — MKURUGENZI wa Mfuko unaosimamia mifuko ya hifadhi za Jamii nchini (SSRA) , Irene Isaka ametoa wito kwa wanachama wapya kujiunga kwa wingi kwenye mifuko hiyo kwa sababu muda si mrefu serikali itaweka uwiano wa mafao sawa kwa mifuko yote.

Isaka alisema hayo jana katika mkutano wa 32 ambao unazikutanisha nchi wanachama wa SADC unaendelea jijini Dar es Salam.

“ Tukiwa katika mkutano huu tunaweza kujifunza mambo mengi kutoka kwa
wenzetu wa SADC huku na
wao wakijifunza mambo kadhaa kutoka kwetu kwani zipo baadhi ya nchi ambazo hazina mfuko mkuu kama SSRA ambao ndio mfuko mama unaosimamkia kazi na utendaji wa mifuko mingine ya kijamii” alisema Isaka.

Aliongeza kwa kusema kuwa hivi sasa kumezuka mtindo kwa badhi ya mifuko ya jamii kujipigia debe, hilo suala ni zuri ila jambo ambalo SSRA tunapingana nalo ni la kunyang’anyana wanachama, hilo siyo jambo zuri hata kama wako kibiashara,” alisema .

Aliongeza kwa kusema kuwa natoa wito kwa mifuko mbalimbali ya kijami kuwa na ushindani endelevu wa kusaidia wanajamii ambao ndiyo wanachama wao.

Aliongeza kwa kusema kwamba SSRA wakiwa wasimamizi wakuu wa mifuko ya hifadhi za jamii wako katika mazungumzo na serikali kuhusu mifuko yote iwe na kikokotoo kimoja kitakachoweka uwiano sawa.

Akizungumzia kuhusu mifuko ya jamii kuwa na kikokotoo kimoja amesema hatua za awali tayari zimekamilika na wameshakusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali huku wakiwa wameshapata Baraka za serikali.

Naye Kamishna wa Bima nchini, Israel Kamuzora alisema mwaka 2009 kulikua na watanzania idadi ya asilimia 6.3 tu ambao walikua wakitumia huduma ya bima tofauti na hivi sasa ambapo mwamko umekuwa mkubwa miongoni mwa watanzania kwa kuona umuhimu wa kukata bima ambazo ni za afya, biashara, magari na nyinginezo.

Akizungumzia watanzania walichojifunza katika mkutano huu kwa nchi zingine,Kamuzora alisema kwamba ni kweli Tanzana iko nyuma kwa pande wa matumizi ya Bima lakini pia tuko mbele kwa nchi kama Msumbiji, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Lesotho na nyinginezo.

Amesema hivi sasa Bima hawacheleweshi malipo kwa watu wanaodai huku akitoa wito kwa wananchi kupeleka madai huku wakiwa na vielelezo vya kutosha.

Alivija vithibitisho hivyo kuwa ni kutoa tarifa haraka zilizokamilika baada ya kupata ajali ikiwa ni ripoti ya polisi,ushahidi wa kipato cha muhusika anachokipata kwa siku ili wao waweze kukokotoa hesabu na muhusika aweze kulipwa.

Aidha alisema kwamba watanzania wengi hawana ajira za kudumu jambo ambalo hukwamisha hesabu za kuharakisha malipo kwa wale ambao hupatwa na ajali na kushindwa kuendelea na kazi zao kama ilivyokua awali.

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Masoko ya Mamlaka ya Masoko,Mitaji na Dhamana (CMSA),Nasama Masinda alisema kwamba Tanzania hatuko katika hatua mbaya huku akizitaja nchi kama Afrika Kusini na Kenya zikiwa zimepiga hatua kubwa.

“Watanzania wamekuwa nyuma huku wakikosa mwamko wa kuchangia katika masoko ya mitaji, hivyo basi tumeweka mikakati ya kutoa elimu kwa umma katika miaka mitano ijayo ili waweze kunufaika na soko la mijati ili nchi iweze kupiga hatua kama jinsi walivyo wenzetu.

Alitolea mfano nchi jiani ya Kenya ambayo ilianza kuwa a soko la mitaji mwaka 1950 huku Tanzania ikianzisha soko hilo 1998.

Mgeni rasmi katika mkutano huo wa sekta ya fedha, soko la mitaji na mifuko ya jamii (CISNA) alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Peter Ilomo.

Ilomo amewataka wajumbe wa mkutano huo wa CISNA watoke na lengo moja la kukuza uhusiano na kuwa na maazimio ya kukuza masoko yao ya mitaji ikiwa ni katika kuvutia wawekezaji waje kununua masoko katika nchi za SADC kwani hiyo ni njia moja wapo ya kukuza uchumi wa Afrika na mwekezaji yeyote hufuata nchi ama umoja wenye nguvu.

“Nchi za SADC zijipange kuwa na ushindani katika nyanja zote za mifuko ya jamii, soko la mitaji na bima ili kuleta maendeleo” alisema Ilomo.

Nchini zilizoshiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na Zimbabwe,Botswana,Tanzania,Angola,Lesotho,Zambia,Malawi,Afrika Kusini,Namibia,Msumbiji,Mautitius na nyinginezo

No comments: