ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 9, 2014

hoja ya haja ....................la Uraia Pacha

wakuu, 
mosi naomba nichukue wasaa huu kukushukuru kwa kazi nzuri ya kutuhabaraisha wana ughaibuni. Unatufikishia habari za nyumbani zinazotufariji tulio mbali na nyumbani. Ankal kabla kuendelea zaidi, napenda niseme machache ya moyoni kutokana na mada nzito ya juzi kutoka kwa kijana wetu mahiri john ,mashaka

naomba pia uniruhusu kusema machache kuhusu mwanazuoni John Mashaka kwa sababu ametugusa kwa mamilioni. na hapana shaka wasomaji wote wa hii blog watakubaliana na mimi kuhusiana na mada zake zinazoonyesha jinsi kijana huyu alivyo na, hekima, upeo na umahiri wa hali ya juu. hakuna swali tena kwamba ndugu mashaka anakubalika kuwa na busara na kipaji cha kipekee. ni mtu mwenye maono na nguvu ya ushawishi. nashawishika kusema kwamba, yeye ni lulu ya tanzania. Alizungumzia kwa ufasaha mkubwa haki zetu watanzania ughaibuni. amediriki kuzungumzia kwa ustadi mkubwa swala ambalo wengi tunaliogopa, ametusemea mamillioni na hatuna budi kumshukuru

kwa kifupi mimi ni mzaliwa wa Kagera. Nimesoma elimu ya sekondari na hata ya kati mkoa wa bukoba. baada ya elimu ya kati, nilijaribu sana kujiunga na chuo kikuu udsm , kusomea uandisi, licha ya kuwa na daraja la kwanza, sikufanikiwa. nilipangiwa kusomea uvetinary kitu ambacho sikupenda, basi nilikaa miaka miwili nikifanya vibarua vya ujenzi hadi mwaka1988. nilitamani sana kuendelea na masomo yangu. Scholarship nyingi zilitolewa na nchi za kigeni, marekani na uingereza, licha ya kuwa na qualifications za kutosha nilinyimwa ila divisheni 3 na hata 4 walipata udhamini katika mazingira tata. 

watu wasiokuwa na qualifications walipewa zile nafasi. basi na mimi kwa vile sikuwa na jina kubwa nyuma yangu sikufanikiwa , nilijitahidi kukusanya vijihela kidogo na hatimaye kuondoka nchini Tanzania kuelekea uturuki, ambako pia nilipigana miezi 5 kukusanya hela za kunifikisha urusi ambako nilitaabika sana kusoma. baada ya kulemewa nililazimika kutafuta uraia ili nipate msaada wa kielimu. Leo ni raia wa Urusi, nimesoma shaada ya kwanza,masters pamoja na phd kwa hela za warusi na kupata kazi Siberia, ambako nimeingia ubia na matajiri kuchimba mafuta. 

Hii inanirudisha kwenye mada ya ndugu Mashaka John. Nilichukua uraia wa urusi ili nipate elimu ambayo Tanzania haikuweza kunipa. Elimu ambayo ilitolewa kwa upendeleo. Leo nataka kurudi tanzania kama mzaliwa wa tanzania anayetambulika kikatiba, lakini kuna baadhi ya wanasiasa wanazuia hilo kutokea.

ninasema wazi kwamba natamani kurudi nchini tanzania na kuwekeza kwenye sekta ya gesi, au nirudi na wawekezaji ambao ntashirkiana nao, lakini nazuiliwa kwa sababu natambulika kama Mrusi.  Ninachosema kwa uwazi ni kwamba, kwa sasa niko tayari kutoa $2million kuwasaidia wagombea wote mkoani Bukoba watakaounga na kutetea haki zetu za kuzaliwa hata kama ni wapinzani. Sijui tafsiri hii itakuwaje lakini, haki yetu sasa lazima tuipiganie. Mimi ni raia wa kirusi kimakaratasi lakini moyoni ni raia wa tanzania

asanteni 
Mdau

E Rwezaura, Siberia

3 comments:

Anonymous said...

wahaya wako juu si mchezo wachaga mko wapi siku hizi jamani,kina mr temba etc

Anonymous said...

safi sana urai wa kitanzania utaupata ndugu wewe ni haki yako naomba na mimi nichonge mchongo wa kuja urusi please

Anonymous said...

tuendelee kudai uraia pacha kwani nami nina kesi kama yako. Nimetokea mkoa ulotokea na nina uraia wa Marekani.