ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 11, 2014

Mourinho apigwa faini na FA.


Meneja wa Chelsea,Jose Mourinho amekosa furaha mara baada ya kupigwa faini na chama cha soka cha nchini Uingereza FA na anatarajia kukata rufaa.
Mourinho alipewa faini ya kiasi cha pauni elfu nane na FA na kuonywa kufuatia kuonyesha utovu wa nidhamu wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Aston Villa mwezi uliopita.
Mreno huyo aliingia uwanjani na kuleta mabishano dhidi ya mwamuzi,Chris Foy mara baada ya mchezo waliofungwa goli 1-0 kwenye dimba la Villa Park mwezi Machi 15.
Mourinho alituma ripoti binafsi ambayo iliangaliwa Jumatano lakini chama hicho kilitazama sheria ya
FA namba(E3) na kuamua kumpa adhabu kutokana na vitendo vyake.
Licha ya maamuzi hayo,Mourinho bado hana furaha kufuatia adhabu hiyo na anasubiri kuandikiwa sababu maalumu ndipo aweze kukata rufaa.
Chelsea walimaliza mechi dhidi ya Villa wakiwa na wachezaji tisa pekee baada ya Willian na Ramires kutolewa nje kwa kadi nyekundu kila mmoja na baadae Mourinho pia alitolewa.
Mourinho tayari aliwahi kuwa na matatizo na FA mapema msimu huu kufuatia kutolewa nje katika ushindi wa goli 4-1 nyumbani dhidi ya Cardiff mwezi Oktoba na alipigwa faini ya pauni elfu nane kwa kosa hilo pia.
Maneno ya meneja huyo baada ya mchezo yalikuwa hivi,”Tunaweza kucheza dhidi ya Aston Villa tena? Hapana nguvu yetu imevunjwa.Kuna mtu amevunja nguvu na kasi.”
“Mechi nyingine tulifungwa kwasababu hatukucheza vizuri.Unatafura sababu ya  halisi kwa kupoteza mchezo.”
Na kuongeza kuwa,”Kama unaenda kwenye mchezo wa Villa,ni ngumu sana.Kilichotokea kwenye kipigo dhidi Villa kamwe siwezi kujifunza na siwezi kukubali.”

No comments: