ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 11, 2014

Smith:Chelsea wanataka kuzikwepa Bayern na Real Madrid.


Mchambuzi mahiri wa soka nchini,Uingereza,Alan Smith anahisi kuwa kupangiwa na Atletico Madrid itakuwa matokeo mazuri zaidi kwa Chelsea katika droo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya Ijumaa.
Kikosi cha Jose Mourinho kilifanikiwa kuitoa Paris Saint-Germain kwa goli la ugenini siku ya Jumanne usiku na kipo katika changamoto kubwa ya kushinda michuano hiyo huku kukisubiriwa droo ya nusu fainali itakayofanyika Nyon.
Smith anaamini kuwa ubora wa safu ya ulinzi ya
Chelsea unawapa nafasi ya kuweza kulitwaa taji hilo jijini Lisbon mwezi Mei 24 lakini anaamini kuwa Bayern Munich na Real Madrid wapo katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa taji hilo.
Huku akisema kuwa,Mourinho huenda akawa na furaha zaidi iwapo atakutana na vinara wa ligi kuu ya Uhispania,Atletico kwenye hatua hiyo ya nne bora.
Na alipoulizwa kuwa timu ipi Chelsea wanataka kuikwepa,mchambuzi huyo alisema kuwa”Bayern namba moja halafu wanafuatia Real Madrid unaweza kupata picha hapo.”
“Hatuwezi kufikiri Chelsea wamekuwa na ubora wa kutosha kwa miaka kadhaa iliyopita na walimaliza kwa kushinda hili.Bado wamepata safu ya ulinzi imara zaidi na sasa wapo vizuri zaidi kwa hilo.”
Smith akaongeza kuwa,”Unaenda kwa njia ndefu kuifunga beki ya kati iliyokuwa na ushirikiano bora wa John Terry na Gary Cahill pamoja na Ivanovic,Azpilicueta na kipa mzuri sana pia yote hayo chini ya meneja mwenye mbinu kali.
“Kama wanazuia kwa jinsi walivyo wanaweza kuwa wagumu zaidi na walichokipata kutoka kwa PSG usiku ule wanapaswa kuanza kuamini jina lao limeandikwa tena kwenye Kombe.”
Lakini akasema Real Madrid dhidi ya Bayern Munich itakuwa kama fainali na anafikiri kuwa kuna timu mbili bora zaidi katika michuano hiyo na utapenda kutaka kuziona timu hizo mbili zikipambana pamoja.
Pia akasisitiza kuwa timu ya Diego Simeone nayo inanafasi nzuri ya kushinda ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza na kudai ushindi walioupata dhidi ya Barcelona siku ya Jumatano haukuwa rahisi hata kidogo.

No comments: