|
Mtoto Satrine akiwa na baba yake hapo jana, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini ©mobile.nation |
Hatimaye mtoto wa mwaka mmoja na nusu Satrine Osinya ambaye risasi
ilituhama kichwani kwake baada ya tukio la mtu asiyefahamika kuvamia
kanisa mjini Mombasa na kufyatua risasi na kuua watu wawili eneo la
tukio na wengine wanne baadae akiwemo mama mzazi wa mtoto huyo, hapo
jana ameruhusiwa kutoka hospitalini alikokuwa chini ya uangalizi wa
daktari baada ya kutolewa risasi hiyo.
Mtoto Osinye alifanyiwa upasuaji tarehe mosi ya
mwezi huu katika
hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya kisha kuwekwa chini ya
uangalizi ambapo hali yake imeendelea vyema na kuanza kucheza kama
ilivyo kwa watoto wengine hali ambayo imeonyesha hali yake iko salama
hivyo madaktari kumpa ruhusa hapo jana.
|
Picha ya mama mzazi wa mtoto huyo, ikiwa juu ya jeneza wakati wa mazishi wiki iliyopita. |
No comments:
Post a Comment