MSANII wa filamu ambaye ni mdogo wa
Kanumba, Seth Bosco hivi karibuni alitinga kanisani akiwa amebeba gitaa
alilokuwa akilitumia Steven Kanumba enzi za uhai wake.
Seth alitinga na gitaa hilo katika
Kanisa la KKKT, Kimara-Temboni kulikokuwa na ibada ya kumbukumbu ya
Kanumba ambapo alionekana akiwa amelishikilia na baada ya ibada alikuwa
akifanya mazoezi ya kupiga gitaa hilo.
“Kanumba alikuwa akilipenda sana
gitaa hili na muda mwingi alikuwa akilitumia kwa kuimba na nyimbo zake
alizorekodi alikuwa akilitumia hili ndiyo maana leo nimeamua kuja nalo
kanisani pia makaburini ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu pia,” alisema
Seth.
No comments:
Post a Comment